
MacDonald Mariga (kushoto) ameshindwa kuisadia Kenya kufuzu hatua ya makundi.
Imechapishwa Agosti 4, 2014, saa 12:37 asubuhi
WAKATI Tanzania ikitupwa nje ya
michuano ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika, AFCON mwakani nchini Morocco
na Msumbiji, Kenya nao walikalia kuti la moto baada ya kufurushwa na Lesotho.
Lesetho walifanikiwa kusonga mbele
katika harakati za kusaka tiketi ya kucheza AFCON 2015 baada ya kutoka suluhu
ya bila kufungana na wenyeji Harambee Stars katika uwanja wa Taifa wa Nyayo
mjini Nairobi jana jioni.
Mechi ya kwanza Lesotho walishinda
bao 1-0 uwanja wao wa nyumbani, hivyo wamewatoa Kenya kwa wastani wa bao 1-0.
Sasa nchi hiyo inaungana na nchi za
Gabon, Angola na wana fainali wa mwaka 2013, Burkina Faso katika kundi C,
ambapo timu mbili za kwanza zitafuzu moja kwa moja kwenda Morocco mwakani.

Robert Sentongo alikuwa shujaa wa Uganda Jana
Nafasi ya Kenya ilikuwa finyu
kwasababu walikosa motisha kutoka benchi la ufundi kwasababu kocha mkuu Adel
Amrouche amefungiwa.
Kocha huyo raia wa Uholanzi
anatumikia kifungo cha mwaka mmoja kwa kitendo chake cha kumtemea mate mwamuzi
wa mechi katika mechi za mapema za kufuzu.
Kocha msaidizi, James Nandwa ndiye
alikiongoza kikosi cha Harambee Stars .
Kama Lesotho watafanikiwa kufuzu
fainali za AFCON 2015, itakuwa mara yao ya kwanza ksuhiriki michuano mikubwa ya
Afrika katika historia yake.
Kwa upande wa Uganda, mambo
yamewanyokea baada ya kufanikiwa kufuzu hatua ya makundi.
Uganda The Cranes walishinda mabao 2-0 katika
mchezo wa kwanza mjini Kampala dhidi ya Mauritania.
Katika mechi ya pili iliyopigwa jana
jioni, Uganda ilishindi bao 1-0 ugenini, hivyo kusonga mbele kwa wastani wa
mabao 3-0.
Bao pekee la Uganda lilifungwa na
Robert Sentongo katika dakika tatu za nyongeza.
0 comments:
Post a Comment