
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Imechapishwa Agosti 4, 2014, saa 11:45 Alfajiri
Shomari Kapombe alilia sana mara baada ya
kumalizika kwa mchezo , na alijitolea kwa muda wote uwanjani , na ilikuwa hivyo
pia kwa wachezaji wengine ambao hawakuamini matokeo ya kuondolewa kwa mara
nyingine na Msumbiji na kufuta ndoto za Watanzania kuiona timu yao ikicheza
fainali za Afrika baada ya miaka 34.
Mwalimu, Nooij alifanya mabadiliko katika nafasi
ya ulinzi wa kushoto baada ya kumuacha nje Oscar Joshua ambaye alionyesha kuwa
mzito katika mchezo wa kwanza na kumuinga mlinzi, Said Mourad.
Stars
ilicheza mfumo wa kujihami lakini kwa kutumia wachezaji wengi wenye kasi.
Erasto Nyini alicheza kama kiungo wa ulinzi akisaidiwa na Mwinyi Kazimoto
ambaye alicheza kama kiungo wa mashambulizi
Msumbiji ilifanya mashambulizi mfululizo kiasi cha
kufanya Stars ‘ kuelemewa’ na kupokea mashambulizi mengi. Krosi kutoka upande
wa kulia wa Stars ilimaliziwa vizuri na mchezaji, Josimar Macheisse katika
dakika ya 45. Hadi nusu ya kwanza inamalizika, Stars ilikuwa nyuma kwa bao 1-0.
Nooij aliamua kuwaanzisha, Thomas Ulimwengu, Hamis Macha, Mbwana Samatta na
John Bocco kwa lengo la kupata bao la mapema, lakini timu ikakosa ‘ balansi’ na
wachezaji wa nafasi ya kiungo wakaonekana kuchoka mapema na kuanza kupoteza
umakini.
Amri Kiemba aliingia mara baada ya kuanza kwa
kipindi cha pili kwa lengo la kuimarisha nafasi ya kiungo. Mcha ambaye alifunga
mabao mawili katika mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita, alishindwa kucheza
vizuri katika wingi, kiasi cha kufanya upande wa kulia kuwa dhaifu.
Nooij
alifanya maamuzi sahihi katika wakati sahihi kwa kumtoa Mcha na kumuingiza
Kiemba lakini alifanya kosa namna ya kuwapanga wachezaji hao wanne. Hakukuwa na
sababu ya kumuanzisha Bocco, kwa sababu haikuwa mechi ya kujaribu.
Stars ilifanya mashambulizi machache katika kipindi
cha kwanza lakini yalikuwa na mipango iliyokamilika. Mourad alikaribia kufunga bao baada ya
kuunganisha vizuri mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Mcha lakini Batte aliokoa
mpira huo uliokuwa ukielekea nyavuni mwanzoni mwa kipindi cha kwanza.
Kabla ya kufungwa bao la kwanza mwamuzi wa pembeni
alimnyoshea kibendera Bocco ambaye alikuwa ‘ on side’ kwa madai kwamba ameotea.
Ilikuwa ni kitendo ambacho kiliwachanganya wachezaji na benchi la ufundi, huku
kocha Nooij akionyesha kulalamika wazi. Ilikuwa ni dakika 44, dakika moja kabla
ya Msumbiji kupata bao.
UKitoa sababu za uchezeshaji mbaya wa waamuzi,
Dennis Batten a wasaidizi wake, Stars ilizidiwa uwanjani kutokana na upangaji
mbaya wa kikosi. Kiemba alionekana kuinua timu na kufanya wachezaji kupiga pasi
na kupanga mashambulizi Samatta alifunga
bao la kusawazisha robo saa kabla ya kumalizika kwa mchezo huo baada ya
kumkimbiza beki wa Msumbiji hadi karibu na lango na kupiga ‘ kiki kali’ iliyomshinda mlinda mlango wa Msumbiji, Dario
Khan


Elias Pelembe ‘ Domingues’ alifunga kwa mkwaju wa
penalti katika mchezo wa sare ya mabao 2-2 wiki mbili zilizopita. Mchezaji huyo
wa klabu ya Kaizer Chiefs alitulia na kupiga kiufundi mpira wa adhabu uliokwenda
moja kwa moja nyavuni na kumshinda kipa Deogratius Munishi baada ya kuangushwa
na Kelvin Yondan nje kidogo ya eneo la hatari. Bao hilo la dakika ya 81
lilimaliza kasi ya Stars ambao walishambulia mfululizo mara baada ya kupata bao
la kusawazisha.
SARE
YA MABAO 2-2, DAR ES SALAAM. Kitendo cha kukubali bao la kusawazisha zikiwa
zimesalia dakika tatu mchezo kumalizika katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
wiki mbili zilizopita ilikuwa ni matokeo nafuu kwa wageni. Msumbiji ilicheza
mchezo wa taratibu ugenini huku wakipanga mashambulizi ya uhakika na kufanikiwa
kufunga mabao mawili ambayo yaliwaweka katika hali ya kujiamini kuelekea mchezo
wa marejeano. Kitendo cha kufunga mabao mawili ya ugenini ambayo kufutwa kwake
ilibidi Stars kufunga mabao mawili, jijini, Maputo jambo ambalo halikuwezekana.
SAFU
YA ULINZI. Shomari Kapombe alionyesha kutojiamini katika mchezo wa kwanza, na
ni hivyo pia ilivyokuwa katika mchezo wa kipigo cha mabao 2-1 siku ya Jumapili.
Mchezaji huyu si mzuri akicheza kama mlinzi wa kulia, si mkabaji mzuri na
hawezi kucheza katika maeneo yake kama mlinzi wa pembeni wakati timu
ikishambuliwa. Ni kweli hakuna namba mbili wa asili kutoka katika klabu 14 za
ligi kuu? Kama safu ya walinzi wa pembeni si imara ni lazima safu ya kati
itayumba.
Kitendo
cha kufungwa mabao nane katika michezo mitatu ni kielelezo tosha kuwa safu ya
ulinzi ni dhaifu, na ili kuiimarisha zaidi ni lazima wachezaji wachaguliwe
kutokana na namba wanazocheza na si wachezaji viraka, Mourad alianza mahali kwa
Oscar. Kelvin Yondan ameendelea kufanya makosa yaleyale.


PASI MKAA. Kupiga pasi ni tatizo kubwa kwa
wachezaji wa Tanzania. Kama mchezaji hutokimbia uwanjani timu haiwezi kucheza
pasi zinazofika. Kuanzia katika ligi kuu hadi michuano ya kimataifa wachezaji
wengi wa Kitanzania wanapiga pasi ' laini' zisizo na nguvu kiasi cha kufanya
wachezaji kucheza kwa spidi ya chini. Msumbiji walikuwa wakipigiana pasi za
nguvu ambazo nyingi zilifika kwa walengwa tofauti na wachezaji wa Stars ambao
walipiga pasi nyingi zisizo na nguvu.
Tanzania
ni moja ya nchi zinazosotea kufuzu kwa fainali za Afrika kwa miongo mitatu sasa
na safari zote zimekuwa na mwisho wa kukatisha tamaa. Stars imefanikiwa
kunolewa na kocha Martin Nooij ambaye ana uzoefu wa kutosha katika soka la
barani Afrika. Nooij aliifundisha Msumbiji kwa miaka miwili na aliisaidia timu
hiyo kufuzu kwa fainali za Afrika, mwaka, 2010, nchini, Angola. Ni kocha mwenye
tamaa ya mafanikio.
Nafasi
ya mshambuliaji, Mbwana Samatta imekuwa tatizo.
Timu pinzani zinaingia uwanjani kwa ajili ya
kumuangalia yeye tu. Bao la kusawazisha katika dakika ya 78 limefikisha ujumbe
kuwa mchezaji ataisaidia sana Stars kama atapangwa katika nafasi ya mshambulizi
wa kwanza. Vipaji vingine kama, Thomas Ulimwengu, Hamis Mcha, na wengineo
vinaweza kutumika katika nafasi nyingine za ushambuliaji. Ukuta mzuri ndiyo
mbinu sahihi ya kushinda mechi. Kutupwa nje kwa Stars ni kutokana na udhaifu
katika ngome. Katika michezo minne iliyopita safu ya mashambulizi imefanikiwa
kufunga mabao saba, huku mabao matano yakifungwa ugenini ni kigezo sahihi ya
maendeleo katika nafasi ya ufungaji. Kumpanga, Samatta kama mshambuliaji wa
pili kumechangia kuondoshwa kwa Stars.
0714
08 43 08
Chanzo: shaffihdauda.com
0 comments:
Post a Comment