
Kitu kambani: Rooney akimalizia vizuri krosi ya Javier Hernandez 'Chicharito' na kufanya matokeo kuwa 1-1 dakika za mapema kipindi cha pili.
Imechapishwa Agosti 5, 2014, saa 11:00 alfajiri
LOUIS van Gaal amefanikiwa kuchukua kombe la mashindano ya kimataifa ya Guinness nchini Marekani kufuatia Manchester United kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya mahasimu wao wakubwa, Liverpool katika mchezo wa fainali uliomalizika usiku wa jana mjini Miami.
Japokuwa kombe hilo sio kubwa kwasababu ni kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, lakini ni heshima kwa Van Gaal na sasa itamuongezea imani kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England inayotarajia kuanza Agosti 16 mwaka huu.
Katika mchezo wa jana, Liverpool walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 14 kwa mkwaju wa penalti uliofungwa na Steven Gerrard.
Bao hilo lilidumu mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinakatika, lakini kipindi cha pili katika dakika ya 55, mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney alisawazisha bao hilo.
Dakika mbili baadaye (57), Juan Mata aliwafungia mashetani hao wekundu bao la pili na la kuongoza na Jesse Lingard alihitimisha karamu ya magoli katika dakika ya 88.
Kitu cha muhimu kwa Van Gaal ni namna timu yake ilivyopambana kutoka nyuma katika dimba la Miami Sun Life na wengine wanaweza kusema ni ushindi ambao haukusthili.
Hii inamaanisha United wanasafiri kurudi nyumbani asubuhi ya leo bila kuonja ladha ya kipigo katika michezo mitano waliyokipiga katika ziara ya Marekani.
Mashindano hayo yalijumuisha timu kubwa kama vile Real Madrid, Roma na Inter Milan.
Kikosi cha MANCHESTER UNITED: De Gea, Evans (Blackett 46), Smalling, Jones, Valencia (Shaw 9), Herrera (Lingard 78), Fletcher (Cleverley 46), Young, Mata (Kagawa 68), Rooney [captain], Hernandez (Nani 68).
Wachezaji wa akiba: Lindegaard, Amos, Johnstone, M Keane, James, Zaha, W Keane.
Wafungaji wa magoli: Rooney (55), Mata (57), Lingard (88)
Kadi ya njano: Shaw (52).
Kikosi cha LIVERPOOL: Mignolet, Kelly, Johnson, Skrtel, Sakho (Toure 74), Gerrard [captain] (Lucas 62), Allen (Ibe 62), Henderson, Coutinho (Peterson 77), Lambert (Can 62), Sterling.
Wachezaji wa akiba: Jones, Coates, Coady, Phillips, Robinson, Suso.
Mfungaji w agoli: Gerrard (14, pen)
Mashabiki waliohudhuria: 51,104

Rooney akitazama mpira unavyozama nyavuni, huku mchezaji wa Liverpool Skrtel akikata tamaa

Shangwe ikaanza: Rooney akishangilia baada ya kuisawazishia United mjini Miami

Kitu cha pili: Juan Mata akishangilia baada ya kufunga bao la pili mjini Miami.

Kasi ya maisha: Mata akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao hilo

Gerrard akipongezwa na Henderson (kulia) na Lambert (kushoto) baada ya kufunga penalti.

Mkongwe: Gerrard akipiga mkwaju wa penalti na kuifungia Liverpool bao la kuongoza katika dakika ya 14 kipindi cha kwanza.
0 comments:
Post a Comment