LIGI kuu soka nchini England imeanza leo kwa mechi saba kupigwa katika viwanja
tofauti.
Mechi ya mapema ilishuhudiwa katika dimba la Old
Trafford ambapo wenyeji Manchester United chini ya kocha mpya, Mholanzi, Louis
Van Gaal walilala 2-1 dhidi ya Swansea City.
Katika mechi nyingine za Jioni, Leicester City
wakiwa nyumbani wamelazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Everton.
QPR wakiwa nyumbani wamechapwa bao 1-0 na Hull
City, wakati Stoke City nao wamelala 1-0 wakiwa uwanja wa nyumbani dhidi ya
Aston Villa.
Katika mechi nyingine West Brom wametoka sare ya
mabao 2-2 na Sunderland.
Tottenham wakiwa ugenini wameshinda bao 1-0 dhidi
ya wenyeji West Ham United.
Mechi ya mwisho leo hii inaendelea baina ya
Asernal dhidi ya Crystal Palace katika uwanja wa Emirates mjini London.
Ligi hiyo itaendelea kesho ambapo washindi wa pili
wa msimu uliopita, Liverpool watakuwa katika dimba lao la Anfield kuchuana na
Sounthampton, wakati mabingwa Manchester City wataoneshana kazi ugenini na
Newcastle United.
Jumatatu ya wiki ijayo, Jose Mourinho ataiongoza
Chelsea kuanza na timu mpya ya Burnley.

0 comments:
Post a Comment