
Na Baraka Mpenja
Imechapishwa Agosti 16, 2014, saa 12:00 jioni
AZAM FC imefuzu robo fainali ya michuano ya kombe
la klabu bingwa ukanda wa Afrika mashariki na kati, maarufu kama Kombe la
Kagame baada ya kuifunga Adamma City ya Ethiopia mabao 4-1 katika mchezo
uliomalizika jioni hii uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali, nchini England.
Mabao ya Azam yamefungwa na John Raphael Bocco ‘Adebayor’,
Didier Kavumbagu ‘Kavu’. Kipre Herman Tchetche na Khamis Mcha ‘Vialli’.
Kwa ushindi huo Azam fc wamefikisha pointi nane katika
nafasi ya kwanza ya kundi A, lakini wanaweza kushika nafasi ya pili kama Rayon
Sport wenye pointi saba watashinda jioni hii.
Wanalamba wametinga robo fainali kwa kushinda
mechi mbili na kutoa sare mbili.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kwa
sare ya bao 1-1 ambapo Azam walikuwa wa kwanza kufunga kupitia kwa Bocco
akiunganisha krosi ya Khamis Mcha ‘Vialli’, lakini Desaleny Bebesh aliisawazishia Adamma katika
dakika ya 39.
Katika dakika 55, Kavumbagu alifunga bao la pili
akimalizia krosi ya Erasto Nyoni.
Dakika ya 60 Mcha alifunga bao la tatu baada ya
kuuwahi mpira uliotemwa na mlinda mlango wa Adamma na katika dakika ya 74
Tchetche alihitimisha karamu ya mabao.
Mchezo unaondelea muda huu ni baina ya wenyeji
Rayon Sport dhidi ya Atlabara kutoka Sudan Kusini.
Kikosi
cha Azam FC leo kilikuwa: Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Gardiel Michael/Said Mourad dk51, David
Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Khamis Mcha ‘Vialli’/Farid Mussa dk61,
Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Mudathir Yahya dk72, John Bocco ‘Adebayor’, Didier
Kavumbangu na Kipre Tchetche.
Waliowakilisha Adama City: Yakoub Fiseha/Yeraswork Terefe dk38, Suleiman Mohamed, Henok
Gemtesa, Demetros Wisilase, Mintesinot Kebede, Wonooson Milkesa, Abreham Yisak,
Ameha Belete, Abdulkerim Abafogi, Desaleny Debesh/Abiy Beyene dk68 na Benyam
Ayele.

0 comments:
Post a Comment