
Khamis Mcha "Vialli' (kulia) yupo kamili gado kuwaua Mambas
Imechapishwa Agosti 3, 2014, saa 6:54 mchana
KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa
Stars, Mholanzi, Mart Nooij imeamua kumuanzisha mfungaji wa mabao wawili katika
mechi iliyopita dhidi ya Msumbiji uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Khamis
Mcha ‘Vialli’ badala ya Mrisho Khalfan Ngassa.
Pia Oscar Joshua ataanzia benchi leo hii na nafasi
yake itachukuliwa na mpiganaji, Said Mourad Mwenda.
Kikosi kitakachoanza leo dhidi ya Mambas:
Deogratius Munish ‘Dida’, Shomar Kapombe, Said Mourad, Kevin Patrick Yondani,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Erasto Edward Nyoni, Thomas Ulimwengu, Mwinyi
Kazimoto, John Bocco, Mbwana Samatta na Khamis Mcha ‘Vialli’.
Wachezaji wa akiba wanatarajiwa kuwa: Aishi
Manula, Aggrey Morris, Oscar Joshua, Haroun Chanongo, Mrisho Ngassa, Simon
Msuva na Amri Kiemba.
Mechi ya kwanza Stars ililazimishwa sare ya mabao
2-2 nyumbani na leo inahitaji kupata ushindi wa aina yoyote ile au sare ya
kuanzia mabao 3-3.
Taarifa kutoka msumbiji zinasema kikosi cha Stars
kipo salama na wachezaji wote wana morali ya kumcharanga Mambas kuanzia majira
ya saa 9:00 alasiri kwa saa za Msumbiji na Tanzania itakuwa saa 10:00 jioni.
Mechi hiyo ya kukata na
shoka itapigwa uwanja wa Taifa wa Zimpeto uliopo nje kidogo ya mji wa Maputo
0 comments:
Post a Comment