.jpg)
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Agosti 3, 2014, saa 6:10 mchana
BAADA ya timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini
ya miaka 17, Serengeti Boys kutolewa katika michezo ya kuwania kufuzu fainali
za Afrika za vijana na Afrika kusini kwa wastani wa mabao 4-0, Rais wa
shirikisho la soka Tanzania, TFF, Jamal Emil Malinzi amekiri kuwa bado timu
haijaandaliwa vizuri.
Rais Malinzi amesema tatizo la timu ni maandalizi
yasiyoridhisha yanayochangiwa na kukosa mfumo sahihi na mpango mzuri wa soka la
vijana.
“Tatizo letu ni lile lile, kwenye maandalizi,
lakini tunapozungumzia maandalizi tunazungumzia uwezo wa kiuchumi, kwamba timu
yetu inaandaliwaje,” Alisema Malinzi.
“Tunaweza kusema timu imejitahidi, Lakini kiukweli
hii ndio mechi yao ya pili ya kimataifa, mechi yao ya kwanza walicheza na
Afrika kusini nyumbani,
“ Kwahiyo lazima sisi tukae kama nchi, kama shirikisho ili tuweze kuangalia programu
zetu za soka la vijana ili watoto kama hawa kabla hawajaingia katika mechi kama
hizi wawe wameshakaa kama timu kuanzia umri wa 12, 13, 14 na 15 , yaani wakae
miaka minne kwenye timu ya taifa,” Aliongeza Malinzi.
Aidha, Rais Malinzi alisema shirikisho hilo
limejipanga upya ili kuhakikisha nchi inakuwa na mfumo sahihi wa soka la
vijana.
“Kipo ambacho kinafanyika, tunaandaa mpango wa
kitaifa wa maendeleo ya soka la vijana na tutazindua mwezi wa 10 mwaka huu, siku
ambayo TFF itatimiza miaka 10 ya kujiunga na FIFA na tutaeleza haya
tunayoyasema ili kama nchi tuwe na mpango endelevu wa soka la vijana,”
0 comments:
Post a Comment