Tuesday, August 19, 2014

507046161XL025_OLYMPIQUE_DEMARSEILLE walifungua vibaya uwanja wa Stade Velodrome baada ya kuchapwa na wageni Montpellier.
Rais wa UEFA, Michel Platini alikuwepo katika uwanja huo, lakini ni mechi ambayo wenyeji kamwe hawataisahau.

Kupoteza mabao 2-0 dhidi ya Montpellier yalikuwa matokeo mabaya na hali ya kisanga cha Andre Ayew kilibaki kuwa gumzo uwanjani.

Nyota huyo wa Ghana katika fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil,  alipata majeraha kichwani kipindi cha kwanza na ilimlazimu kubadilisha jezi baada ya damu kutawala katika jezi yake na aliendelea na mechi.

Kipindi cha pili, bandeji katika jeraha hilo ilitoka na damu kuanza kutoka na kuchafua jezi yake na ikambidi abadili tena. Lakini kulikuwa na tatizo.

Marseille walikuwa na jezi zake mbili tu namba 10 mgongoni na yatari alikuwa ameshazichafua zote kwa damu.

(Screencap thanks to Alex Baker)

Ayew alionekana katika TV ya uwanjani akiwa amechukizwa na kitendo hicho
Mtunza vifaa wa klabu hiyo alitoa jezi namba 33, lakini kwa kuwa Ayew alianza mechi kwa kuvaa jezi namba 10, alitakiwa kumaliza mechi kwa namba hiyo hiyo.

Kwahiyo, timu ilijaribu kufuta namba 33 na kuandika namba 10, lakini jitihada ziligonga mwamba, kwahiyo Marseille ikabidi wamtoe Ayew katika dakika ya 52 baada ya kukosa jezi. Hali hii ilimchefua sana kocha Marcelo Bielsa.

Hakuna aliyemtia moyo, Ayew alirudi benchi akiwa hana jezi yoyote.



0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video