.jpg)
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Agosti 4, 2014, saa 1:26 usiku
RAIS mstaafu wa klabu bya Simba sc, ambaye ni mbunge
wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage imelazwa Hospitali ya mkoa wa Dodoma baada ya
kupata ajali ya gari akitokea Tabora kueleka mjini Dodoma leo.
Imeelezwa kuwa Rage alikuwa anakwenda Dodoma
kuhudhuria vikao maalumu vya bunge la katiba.
Ajali hiyo imetokea eneo la Chigongwe mkoani Dodoma.
Ajali hiyo imetokea eneo la Chigongwe mkoani Dodoma.
Imeripotiwa kuwa katika gari hilo, Mheshimiwa Rage
alikuwa na abiria wengine ambao ni mbunge wa viti maalumu, Munde Tambwe, Issa Chimwaga , Mwanahamisi
Ramadhani na Dereva John NKoya.
Abiria wote walipata majeruhi, isipokuwa dereva wa
gari hilo, lakini wanaendelea kupata matibabu na hali zao zinakwenda vizuri.
Rage amezungumza akiwa wodini mkoani Dodoma, na
kueleza kuwa amepata majeraha katika bega la mkono wa kushoto na eneo la nyuma
ya mgongo.
Rage aliongeza kuwa ajali hiyo imetokea wakati
dereva wa gari lao akijaribu kulipita roli, lakini ghafla dareva wa Roli hilo
akaingia katikati ya barabara na ikamlazimu dereva wao kwenda pembeni ya barabara
na gari kupinduka na kutumbukia kwenye korongo.
Mtandao huu unafuatilia taarifa kamili kuhusu
ajali hiyo.
Ugua pole mwanamichezo Rage na abiria wengine wote.
Ugua pole mwanamichezo Rage na abiria wengine wote.
0 comments:
Post a Comment