
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Agosti 2, 2014, saa 12:06 jioni
KLABU ya Simba sc inatarajia kufanya mkutano mkuu
wa wanachama kesho Agosti 3 mwaka huu katika ukumbi wa Police Officers Mess
Oysterbay, jijini Dar es salaam.
Mkutano huo wa kwanza kufanyika chini ya viongozi
wapya wanaoongozwa na Rais Evans Elieza Aveva na makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’
utafanyika ukiwa na agenda 13 za kujadili.
Agenda inayotarajia kuwa moto wa kuotea mbali ni
ile ya wanachama 72 waliosimamishwa na
kamati ya utendaji akiwemo aliyekuwa mgombea wa Urais Komred, Michael Richard Wambura.
‘Kidume’ Wambura alisimamishwa uanachama wake
mwaka 2010 kutokana na kosa la kuipeleka klabu mahakamani.
Wanachama wengine 69 wanakabiliwa na kosa kama
hilo kwani waliipeleka klabu mahakamu kuu wakitaka kusimamishwa kwa uchaguzi
mkuu uliofanyika juni 29 mwaka huu kwa madai kuwa katiba ilikiukwa.
Agenda ya kwanza katika mkutano wa kesho ni kuhakiki
wanachama wanaohudhuria mkutano na agenda ya pili ni kuthibitisha Agenda za
mkutano huo.
Agenda ya tatu katika mkutano huo utakaotoa hatima
ya Wambura ni kuthibitisha kumbukumbu za kikao kilichopita na Agenda ya nne ni
Yatokanayo na kumbukumbu ya kikao kilichopita.
Agenda ya tano ni hotuba ya Rais wa Simba, Evans
Aveva na agenda ya sita ni kupokea na kujadili taarifa kutoka kamati ya
utendaji.
Agenda ya saba ni kuthibitisha bajeti ya mwaka ya
klabu, wakati agenda ya nane ni
kuthibitisha uteuzi wa wakaguzi wa hesabu wa nje.
Agenda ya tisa ni kuthibitisha walezi na wadhamini
wa klabu, wakati agenda ya kumi ni marekebisho ya katiba.
Agenda ya 11 inayotarajiwa kuwa ya vuta ni kuvute
ni ile kuhusu wanachama 72 waliosimamisha na kamati ya utendaj.
Baada ya hapo, agenda ya 12 ni wanachama wa
heshima na agenda ya 13 na ya mwisho ni kufunga kikao.
0 comments:
Post a Comment