Saturday, August 16, 2014

Imechapishwa Agosti 16, 2014, saa 5:34 asubuhi

CRISTIANO Ronaldo ameupinga mjadala unaoendelea kwasasa kuwa mchezaji mwenzake wa Real Madrid, mlinda mlango, Iker Casillas zama zake zimepita.
Ronaldo amesisitiza kuwa nahodha huyo wa Hispania bado yupo katika ‘Kiwango cha dunia’.

Kipa huyo alikabiliwa na misimu miwili migumu baada ya kupoteza namba mbele ya Diego Lopez na kuonesha kiwango cha chini katika fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil na kushuhudia Hispania ikitolewa hatua ya makundi.

Licha ya kiwango chake cha karibuni, kuuzwa kwa Lopez katika klabu ya AC Milan kunamrejesha Casillas kama kipa namba moja mbele ya kipa mpya aliyesajiliwa, Keylor Navas.

Ronaldo alisema timu itakuwa katika mikono salama chini ya kipa huyo mwenye miaka 33 ambaye ameshinda makombe matatu ya UEFA, mawili ya mashindano ya Ulaya na kombe la dunia.

“Iker hajawahi kutoka katika orodha ya makipa bora wa dunia,” Ronaldo aliwaambia waandishi. “Siku zote amekuwa katika kiwango cha dunia”.

Madrid walifungua pazia la UEFA kwa kutwaa kombe la ‘UEFA Super Cup’ dhidi ya Sevilla, huku Ronaldo akifunga mabao yote mawili katika ushindi wa 2-0 na Mreno huyo alisisitiza kuwa kombe hilo ni mwanzo tu wa kutetea ubingwa wa UEFA.


Vijana hao wa Carlo Ancelotti wanaendelea na maandalizi ya msimu na leo watakuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya Fiorentina kabla ya kuanza mchezo wa ufunguzi wa La liga dhidi ya mahasimu wao, Atletico Madrid jumanne ijayo.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video