Saturday, August 16, 2014

Kazi imeanza: Luis Suarez akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa  Barcelona leo ijumaa akiwemo nahodha wa klabu, Xavi.

Imechapishwa Agosti 16, 2014, saa 5:30 asubuhi

BAADA ya kuanza mazoezi na wachezaji wenzake wa Barcelona kwa mara ya kwanza jana ijumaa, Luis Suarez amesema ni muda wa kusahau miezi miwili iliyopita.

Siku ya Alhamis, mahakama ya juu ya rufani ya michezo ya CAS alitangaza kuwa kifungo cha miezi minne cha Luis Suarez kujihusisha na shughuli za michezo kisijumuishe na kutoshiriki mazoezi.

FIFA walimfungia Muuruguay huyo baada ya kumng’ata beki wa Italia, Giorgio Chiellin katika fainali za kombe la dunia-na hii ilikuwa mara ya tatu kukutwa na hatia ya kosa la aina hiyo.

Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Barcelona akitokea Liverpool kwa dau la paundi milioni 75 alianza mazoezni na kikosi cha Barcelona ijumaa na anaweza kucheza mechi ya kwanza siku ya jumatatu katika mechi ya kirafiki dhidi ya Leon kwenye uwanja wa Camp Nou.

“Nina furaha kubwa ya kucheza tena mpira na wachezaji wenzangu,” Suarez aliiambia Tovuti ya Barca.

“Hali ya kutocheza ilinikosesha raha. Ninajutia makosa niliyoyafanya na niliomba msamaha, lakini haya yasahaulike”.


“Tufikirie ya baadaye katika klabu yangu ya Barcelona, klabu niliyoota kuichezea”.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video