Imechapishwa Julai 9, 2014, saa 7:45 mchana
WAKATI dunia nzima ikisubiri
kwa hamu nusu fainali ya pili ya kombe la dunia baina ya Argentina dhidi ya Uholanzi,
wadau na wapenzi wa soka wameendelea kutoa utabiri wao.
Kila mdau anatoa sababu za
kuipa timu fulani ya kuibuka na ushindi, japokuwa wataalam wa soka wakakwambia
mpira ni dakika 90.
Jana Brazil wameingia katika
rekodi mbaya zaidi ya soka la dunia baada ya kufungwa mabao 7-1 na Ujerumani na
kuwa timu ya kwanza kufungwa mabao mengi zaidi katika hatua ya nusu fainali tangu
kombe la dunia lilipoanza mwaka 1930 nchini Uruguay.
Mtandao huu umehojiana na
baadhi ya wadau kutoka hapa nchini na nje ya nchi, lengo ni kutaka kujua ni timu
gani inapewa nafasi ya kushinda.
Songa na utabiri hapa chini………………..
ANUARY MKAMA KUTOKA NCHINI
UJERUMANI

“Mechi itakuwa ngumu ila
Argentina kumkosa Di Maria ni pengo kubwa sana ambalo litaiathiri timu hiyo
kama unavyojua mashambulizi ya Argentina yanamtegemea Messi na Di Maria, ila
nategemea Uholanzi kushinda kama ilivyofanya katika fainali za mwaka 1998 kwasababu
ina wachezaji wenye uchu wa magoli wakiongozwa na Robben na Van Persie kitu
muhimu ambacho Van Gaal anachangamoto ni kuhakikisha safu yake ya kiungo
inampelekea mipira zaidi Van Persie”.
Kuhusu uwezo wa mchezaji kuamua matokoea, Mkama anasema “yaah
kweli, ila Uholanzi wako vizuri zaidi na fainali itakuwa nzuri wakicheza
na ujerumani”.
NELLYNICE MNYIRAMBA-DAR ES SALAAM TANZANIA

“ARGENTINA OUT. Sometimes kiingereza kinaleta ladha kukazia
kitu maana sioni njia ya Argentina kuepuka kichapo kutokana na beki zao
kukatika sana, ingawa hawajafungwa goli nyingi ni kutokana na forward walizokutana
nazo, but kwa forward line ya Uholanzi
sina shaka wanawatungua Argentina kilaini sana. Uholanzi 3 Argentina 1”.
PETER MABERE a.k.a Boko-DAR ES
SALAAM TANZANIA

“Mi natabiri Argentina
watashinda mechi ya leo japokuwa mechi itakuwa ngumu sana, ni nusu fainali ya
pili inayozikutanisha timu zenye utamaduni tofauti kabisa wa soka, Argentina
inayotoka bara la amerika ya kusini ikiwa na utamaduni wake wa soka, lakinI pia uholanzi inayotoka bara la ulaya na
falsafa tofauti kabisa na soka la Amerika ya kusini. Lakin pia tusisahau kuwa
timu zote zinaundwa na nyota ambao wana uwezo binafsi ( individual talent) kama
mchezaji bora wa dunia mara nne Lionel Andres Messi, lakin pia winga wa fc Bayern munich mdachi
Arjen Robben, hawa ndio wachezaji ambao kimsingi ukiachilia mbali ushirikiano
wa timu ( team work) bado wanaweza kuamua mchezo huu. Lakin nazitazama safu za
ulinzi za timu zote mbili nagundua kuwa safu ya ulinzi ya Uholanzi inayoongozwa
na Vlaar itapata wakati mgumu sana wa kuwazuia washambuliaji Gonzalo Higuain na
Sergio Aguero ambaye amerudi baada ya kusumbuliwa na majeraha. Hiyo ndiyo
sababu ya msingi inayonipa kiburi cha kutupa karata yangu kwa Argentina kuwa
ataondoka kidedea katika nusu fainali ya leo kaka”.
KASSIM MTOLEA-MWANZA TANZANIA

“Mi natabiri kwamba mchezo utakuwa mgumu lakini kura
nawapata Uholanzi kuibuka na ushindi katika mchezo wa leo”.
MFUNGO JUNIOR- KATAVI TANZANIA


Leo anakufa Holland anakufa
2.........kwanza hofu imetanda juu ya Van Persie hayuko fit ukiangalia ni mmoja
wa watu tegemeo, Argentina iliyoundwa kumzunguka Messi wana uwezo wa kupenya
ngome yoyote kwani Messi ana uwezo wa kupunguza mabeki hata wa 3 na kurejea kwa
kun Aguero ni boost kubwa kwenye kikosi cha Argentina na mwisho licha ya
uhasama uliopo Amerika kusini, lakin natumaini atapata sapoti kubwa leo ili
aweze kulibakisha kombe kwenye ardhi ya Amerika kusini".
FRANCIS KIVUYO-DAR ES SALAAM TANZANIA

“Argentina haina tofauti kubwa na Brazil, wana tabia ya
kumtegemea mchezaji mmoja(Mesi)..kwa ujumla timu ya Argentina ina makundi.
Lakini kwa upande wa uholanzi, kuna watu hatari kabisa pale mbele.....roben &
van Persie ambao wana wining mentality muda wote wakiwa uwanjani, vilevile
wachezji wa Uholanzi hupenda kucheza kama timu(total football) kwa hiyo kwa
mchezo wa leo Argentina ndo mwisho wake!”
SELEMAN PHARLES MABALA (pichani kushoto)-DAR ES
SALAAM TANZANIA
Tukutane baada ya mechi.................stay tuned!



0 comments:
Post a Comment