
Muda wa pati ukawadia: Wachezaji wa Uholanzi wakipozi katika picha huku wakiwa na medali zao baada ya kuitandika Brazil mabao 3-0 na kushika nafasi ya tatu katika fainali za kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Mshindi: Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal akipokea medali kutoka kwa rais wa FIFA, Sepp Blatter.

Ndoto zilianzia hapa: Nahodha wa Uholanzi, Robin van Persie alifunga bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati na kumuacha kipa Julio Cesar akiambulia unyoya tu. Chezea RVP weyeeeeeeeeeeeee!

Maboya: Kipa wa Brazil, Julio Cesar akishindwa kuokoa penati ya Robin van Persie katika dakika ya 3 ya kipindi cha kwanza.

Oyooo! wamekalishwa tena! : Robin van Persie akishangilia bao lake na mchezaji mwenzake Dirk Kuyt (aliyempanda juu)

Hesabau tu!: Beki wa Uholanzi, Daley Blind akipiga shuti kuandika bao la pili dhidi ya Brazil.

Freshi sana wana!: Daley Blind (wa pili kushoto) akishangilia baada ya kuifungia Uholanzi bao la pili dhidi ya Brazil

Beki wa Uholanzi alipata majeraha wakati akichuana na Oscar wa Brazil (kushoto).

Beki aliyejeruhiwa akiwa amepata lifti ya machela

Kingine hicho: Kiungo wa Uholanzi, Georginio Wijnaldum akifunga bao la tatu na la ushindi katika dakika za majeruhi.

Kaah! si majanga haya jamani, umefanya nini Georginio Wijnaldum?

Usiku wa maajabu: Majeruhi Neymar hakuweza hata kutazama mechi hiyo.
0 comments:
Post a Comment