RAIS mpya wa klabu ya Simba sc, Evans Elieza Aveva alipata kura 1,455 dhidi ya mpinzani wake
Andrew Peter Tupa, aliyepata kura 388.
Mjumbe
wa Kamati ya Uchaguzi na aliyesimamia zoezi hilo, Amin Bakhresa, wakati
akitangaza matokeo hayo alisema kuwa mshindi wa nafasi ya Makamu wa Rais ni
Geofrey Nyange 'Kaburu' aliyepata kura 1,046 na kuwashinda Jamhuri Kihwelu
'Julio' (412), Swedy Mkwabi (373) na Bundala Kabula kura 25.
Wagombea watano waliochaguliwa kuunda Kamati ya Utendaji ni Iddi Kajuna aliyepata kura 893, Said Tully (788), Collins Frisch (758), Ally Suru ( 627) na kwa upande wa mwanamke aliyeshinda ni Jasmine Badour alyepata kura 933 na kuwashinda Asha Muhaji aliyepata kura 623 na Amina Poyo (330).

SAFU YA MPYA YA UONGOZI WA SIMBA SC
INASIMAMA HIVI
RAIS-EVANS ELIEZA AVEVA
MAKAMU WA RAIS-GEOFREY NYANGE KABURU
WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI-IDDI
KAJUNA, SAID TULLY, COLLINS FRISCH, ALLY SURU NA JASMINE BADOUR
0 comments:
Post a Comment