
Andrey
Coutinho akisaini mkataba wa kuitumikia Yanga kwa kipindi cha miaka miwili
mbele ya Katibu Mkuu Beno Njovu leo makao makuu ya klabu
Kiungo
mshamabuliaji Andrey Marcel Ferreira Coutinho raia wa Brazil leo amesaini
mkataba wa miwili kuitumikia timu ya Young Africans kwa ajili ya michuano
mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya Kombe la
Shirikisho barani Afrika.
Katibu
mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema usajliwa mchezaji Coutinho
ni sehem ya muendelezo wa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu na kama
ilivyokawaida wao mambo yao ni kimyakimya.
Coutinho
ambaye alizaliwa tarehe 12 Januari 1990 amekulia kwenye mji wa Berem ambapo
alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Paysandu Sports Club kabla ya
kwenda nchini Asia katika nchi ya Myanmar katika klabu ya Rukhapura United.
Mpaka
anajiunga na klabu ya Young Africans Andrey Coutinho alikuwa akichezea timu ya
Castanhal EC iliyopo kwenye Ligi Daraja la pili ambao aliweza kuichezea kwa
michezo yote ya mzunguko wa pili mwaka 2014.
Katika
hatua nyingine kikosi cha Young Africans kinatarajia kuendelea na mazoezi kesho
chini ya kocha Marcio Maximo katika ufuke wa Coco Beach ikiwa ni siku yake ya
kwanza na jioni katika Uwanja wa Bandari Tandika kuanza kazi baada ya leo kuwa
na mkutano wa ndani na wachezaji wake pamoja na benchi la ufundi.
0 comments:
Post a Comment