
Katua: Ander Herrera amesajiliwa na Manchester United akitokea Athletic Bilbao kwa dau la paundi milioni 28.8 jana alhamisi.
Manchester
United imeamua kutumia kitita cha paundi milioni 58.8 kwa ajili ya
kumsajili Luke Shaw na Ander Herrera, ikiwa ni malengo ya kurejea juu
katika michuano ya ligi kuu England.
United
itakamilisha dili la paundi milioni 30 kumnasa beki wa kushoto wa
England, Shaw, leo ijumaa ikiwa ni saa 24 zimepita tangu wamsajili
kiungo wa Atletico Madrid, Herrera kwa dau la paundi milioni 28.8.
Mkurugenzi
msaidizi wa Man United Ed Woodward ametoa paundi milioni 60 za haraka
haraka ili kufanya usajili huo na kuepuka makosa yaliyojitokeza majira
ya kiangazi ya usajili mwaka jana na amesema hataishia hapo, bali
atahitaji kusajili angalau wachezaji wapya wawili.

Kitu kinatua Old Trafford: Luke Shaw anatarajiwa kuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Man United kwa dau la paundi milioni 30m leo ijumaa.

Biashara: Kocha wa Man United, Louis van Gaal atakuwa na Herrera na Shaw msimu ujao.
HISTORIA YA WACHEZAJI HAO
ANDER HERRERA, Kiungo, Umri 24
2008-2009: Zaragoza B (alicheza mechi 10, alifunga magoli 2)
2009-2011: Zaragoza (alicheza mechi 82, alifunga mabao 6)
2011-2014: Athletic Bilbao (alicheza mechi 94, alifunga magoli 7)
2014-Kwasasa: Manchester United
LUKE SHAW, Beki wa kushoto, miaka 18
2012-2014: Southampton (alicheza mechi 60 , hajafunga goli lolote)
2014-kwasasa: England (amecheza mechi 3, hajafunga bao lolote)
2008-2009: Zaragoza B (alicheza mechi 10, alifunga magoli 2)
2009-2011: Zaragoza (alicheza mechi 82, alifunga mabao 6)
2011-2014: Athletic Bilbao (alicheza mechi 94, alifunga magoli 7)
2014-Kwasasa: Manchester United
LUKE SHAW, Beki wa kushoto, miaka 18
2012-2014: Southampton (alicheza mechi 60 , hajafunga goli lolote)
2014-kwasasa: England (amecheza mechi 3, hajafunga bao lolote)
Japokuwa Southampton walikuwa wanahitaji paundi milioni 40 kwa nyota huyo mwenye miaka 18, lakini Man United wamewashawishi kwa paundi milioni 30 na leo hii itafanyiwa vipimo vya afya kwenye uwanja wa Carrington kabla ya kusaini mktaba wa miaka mitano.
0 comments:
Post a Comment