

HATUA ya Makundi ya kombe la dunia linaloendelea
kushika kasi nchini Brazil imekamilika jana na kushuhudia timu mbili za Afrika
zikitinga hatua ya 16.
Sare ya bao 1-1 baina ya Algeria dhidi ya Urusi
imewafanya wanaume hao wa Afrika kufuzu hatua ya mtoano, lakini Nigeria
walikuwa wa kwanza kufuzu licha ya kufungwa mechi ya mwisho mabao 3-2 dhidi
Argentina.
Timu za Cameroon, Ivory Coast, na Ghana
zimeshafungasha virago.
Ratiba ya mtoano itashuhudia timu za Afrika zikivaana na
mabingwa wa zamani wa michuano hiyo mikubwa katika ulimwengu wa soka.
Nigeria maarufu kama Super Eagles watachuana na
Ufaransa ya akina Karim Benzema.
Algeria watakuwa na kibarua kikali dhidi ya
Ujerumani ya Thomas Muller.
Mechi nyingine zitawakutanisha wenyeji Brazil
dhidi ya Chile, Colombia dhidi ya Uruguay, Uholanzi na Mexico, Argentina na
Uswisi, Ubelgiji wao watachuana na Marekani.
0 comments:
Post a Comment