
Safari ya miaka minne ya mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage inafikia kikomo leo
Na
Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
SIMBA
SC wapo katika mkutano mkuu wa Uchaguzi unaoendelea muda huu katika Ukumbi
wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Uchaguzi huo unashirikisha jumla ya wagombea 27 ambapo
nafasi ya juu kabisa, Urais, inawaniwa na wagombea wawili Evans Elieza Aveva na
Andrew Peter Tupa.
Nafasi ya Urais inawaniwa na Swedi Mkwabi, Bundala
Kabulwa ,
Geofrey Nyange `Kuburu` na Jamhuri Musa Kihwelo `Julio`.
Geofrey Nyange `Kuburu` na Jamhuri Musa Kihwelo `Julio`.
Wanaowania ujumbe wa kamati ya utendaji ni Said Tulliy, Yasini Mwete, Ally Suru,
Rodney Chiduo, Said Pamba, Ally Chaurembo , Abdulhamid Mshangama , Chano
Almasi, Damian Manembe, Ibrahim Masoud, Kajuna Noor, Hamisi
Mkoma, Alfred Elia na Saidi Kubenea.
Wagombea wengine ni Idd Mkamballah, Juma Mussa, Maulid
Abdallah na Collin Frisch. Wagombea.
kwa upande wa wanawake ni Asha Muhaji, Amina Poyo na Jasmine Badour.
kwa upande wa wanawake ni Asha Muhaji, Amina Poyo na Jasmine Badour.
Mchakato huu wa
uchaguzi umefika hapa ulipo baada ya kugubikwa na mizengwe kadhaa.
Inafahamika kuwa
matatizo yalianza siku alipoenguliwa mgombea wa nafasi ya Urais Michael Richard
Wambura.
Wambura
alienguliwa na kamati ya uchaguzi ya Simba sc, chini ya mwenyekiti wake, Wakili
Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kwa sababu ya kuipeleka Simba mahakamani na
kusimamishwa uanachama mwaka 2010.
Lakini `kidume`
alikata rufaa katika kamati ya rufani ya uchaguzi ya TFF chini ya mwenyekiti
wake, Jaji Julius Mutabazi Lugaziya.
Kamati ya jaji
Lugaziya alimrejesha Wambura kuendelea na mchakato wa uchaguzi baada ya
kubainika kulikuwa na makosa yaliyofanywa na Simba kwa kumuacha Wambura
aendelee kufanya shughuli za klabu kama mwanachama akiwemo kulipa ada wakati
walimsimamisha.

Lakini kamati ya
Ndumbaro alimuengua kwa mara ya pili kwa sababu ya kupiga kampeni kabla ya
muda. Wambura alikata rufaa tena katika kamati ya uchaguzi ya TFF, lakini
rufani yake ilikataliwa, hivyo kutoka rasmi kwenye mchakato wa uchaguzi wa Simba
sc.
Baada ya tukio
hilo, baadhi ya wanachama wa Simba walienda kufungua kesi mahakama kuu wakitaka
mahakama isimamishe uchaguzi kwasababu Wambura hakutendewa haki.
Mahakama Kuu
ilikataa kusimamisha uchaguzi huo, na hatimaye leo hii rais mpya, makamu wa
rais na wajumbe wa kamati ya utendaji wanapatikana.
Ilikuwa safari
ndefu na wengine waliamini isingetimia, lakini hatimaye kitendawili
kimeteguliwa.
Kazi kwenu
wanachama wa Simba. Kwa muda sasa mmesikiliza kampeni za wagombea wote.
Kinachotakiwa ni kutuliza akili kwenye maboksi ya kura ili wapatikane viongozi
sahihi.
Inafahamika wapo
ambao wanaumia kwasababu wagombea wanaowaunga mkono walienguliwa hususani
Wambura, lakini yameshatokea na mwisho wa siku Simba ni yenu na mnatakiwa
kushirikiana kupata viongozi wapya.
Simba inahitaji
mabadiliko makubwa, na kwa kuanza, leo ni siku muhimu kwa wanasimba wote.
Zaidi mtandao huu
na timu yake unawatakia kila la heri katika uchaguzi wenu unaofanyika leo.
0 comments:
Post a Comment