
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
UCHAGUZI mkuu wa klabu ya Simba sc umemalizika
salama licha ya changamoto kadhaa kujitokeza na sasa zoezi linaloendelea ni
kumalizia kuhesabu kura za wagombea wa nafasi za ujumbe.
Kwa nafasi ya Urais, tayari mambo yameshafahamika
ingawa taarifa rasmi kutoka kamati ya uchaguzi haijatangazwa.
Evans Elieza Aveva ni rais wa kwanza wa klabu ya
Simba kwani matokeo ambayo sio rasmi yanaonesha ameibuka na ushindi mkubwa.
Aveva amepata kura 1461, huku mpinzani wake pekee,
Andrew Peter Tupa akipata kura 381.
Wagombea hawa walikuwa na uzito tofauti, kwasababu
dalili za Eveva kushinda zilianza siku aliyoenda kuchukua fomu.
Hata hivyo ilionekana kungekuwa na mchuano mkali
endapo Michael Richard Wambura angeendelea na uchaguzi.
Nafasi ya makamu wa rais, aliyewahi kuwa makamu
mwenyekiti wa Simba katika uongozi unaomaliza muda wake, Geofrey Nyange `Kaburu`
kwa matokeo yasiyo rasmi ameshinda nafasi hiyo.
Matokeo rasmi yatatangazwa muda wowote kutoka
sasa, endelea kufuatilia mtandao huu.
0 comments:
Post a Comment