Frank Domayo `Chumvi` amesaini mkataba wa miaka miwili Azam fc
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Uongozi
wa klabu ya Young Africans unapenda kuwajulisha wanachama wake, wapenzi wa soka
na wadau kwa ujumla kuwa taarifa za kuhama kwa wachezai wake Didier Kavumbagu
na Frank Domayo kwenda kujiunga na Azam FC zisiwakatishe tamaa, ni mapenzi ya wachezaj
wenyewe kwani walishakubaliana na uongozi kila kitu juu ya kuendelea kuitumikia
Yanga kabla ya siku mbili hizi kuonekana wakiwa wamejiunga na wana ramba ramba.
Yanga
tayari ina wachezaji watatu wenye mikataba inayoendelea na kama kanuni za VPL
kwa wachezai wa kimataifa kuwa watatu zitatumika wachezaji Haruna Niyonzima,
Hamisi Kizza na Emmanuel Okwi ndio watakaoendelea, hivyo uongozi uliomba
mwongozo kwa TFF juu ya taratibu zitakazotumika kwa msimu ujao kabla ya
kuwasainisha Kavumbagu na Twite.
Awali
uongozi wa Yanga ulikuwa kwenye mazungumzo na wachezaji hao tangu mwanzoni mwa
msimu wa 2013/2014 juu ya kuongezewa muda wa mikataba yao ili waweze kuendelea
kuitumika Yanga kwa ajili msimu mpya ujao 2014/2015.
Didier
Kavumbagu na Mbuyu Twite ambao mikataba yao ilikuwa mwishoni waliongea na
uongozi tangu mapema mwaka jana mwezi wa Septemba juu ya kuweka sahihi zao na
kuendelea kuitumikia Yanga na kukubaliana mambo yote ya msingi kikubwa
kilichokuwa kinasubiriwa ni maamuzi ya TFF juu ya usajili wa wachezaji wa
kigeni msimu mpya wa 2014/2015 kwani Azimio la Bagamoyo linapaswa kuanza
kutekelezwa msimu huu
Uongozi
wa Yanga uliandikia TFF barua mapema kuomba kupewa mwongozo wa kanuni
zitakazotumika kwenye usajli kwa wachezaji wa kimataifa kwa msimu mpya kufuatia
Azimio la Bagamoyo kuelekeza msimu huu kila timu inapasa kuwa na wachezaji
watatu wa kigeni, mpaka sasa uongozi wa Yanga haujapata majibu juu ya utaratibu
utakaotumika kwenye msimu wa Ligi Kuu ijayo.

Didier Kavumbagu amesaini mkataba wa mwaka mmoja Azam fc
Hivyo
makubaliano ya wachezaji Didier Kavumbagu, Mbuyu Twite na uongozi wa Yanga SC
yalikua yakisubira majibu ya TFF juu ya kanuni zipi zitakazotumika kwenye
usajili msimu wa 2014/2015 kwa wachezaji wa kigeni na katika hali ya kushangaza
Kavumbagu akaonekana tayari ameshasaini kuichezea timu ya Azam FC.
Kuhusu
Frank Domayo aliyeripotiwa jana kujiunga na Azam FC pia alikuwa katika
makubaliano ya kuongeza mkataa tangu mwezi Julai 2013, alikubaliana na uongozi
juu ya mambo yote ya msingi na kilichobakia ilikuwa ni kuweka sahihi kwenye
mkataba mpya, lakini Domayo alisema hawezi kusaini mpaka siku atakapokuja
mjomba wake ambaye ndie wakala wake na ahadi hiyo iliendelea kwa muda wa mwaka
mzima kabla ya jana kusikia ameshasaini timu nyngine.
Habari
hizi zimewashitua wapenzi, wanachama na washabiki wa Young Africans lakini
ukweli ni kuwa wachezaji wenyewe walisindwa kuwa wakweli kwa viongozi na mwisho
wa siku walikua na mipango yao ya kuondoka, hivyo uongozi ulijtahid kadri ya
uwezo wake lakini wachezaji wanaonekana hawakua tayari kuendelea kuichezea
Yanga SC.
Taarifa
kamili kuhusu mipango ya timu kwa msimu ujao pamoja na ripoti ya kocha mkuu
Hans pamoja na benchi lake la Ufundi zitatolewa hivi karibuni baada ya benchi
la ufundi na uongozi kukaa kwa pamoja na kuafikiana mipango ya msimu ujao.
Aidha
uongozi wa Yanga SC unawaomba wanachama wake, wapenzi na washabiki wasiwe na
wasi wasi juu ya kuondoka kwa wachezaji hao kwani Yanga bado ina nafasi
wachezaji wengi wenye vipaji na itaendelea kuboresha kikosi chake kwa
kuzingatia maelekezo ya kocha mkuu Hans katika usajli wa msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment