NYOTA
wa zamani wa Barcelona, Deco, amesema kushuka kwa kiwango cha klabu hiyo kama
klabu bora ya kihistoria duniani ilitarajiwa.
Vijana
wa Gerardo Martino hawako katika kiwango kama misimu ya nyuma na msimu huu walitolewa
hatua ya robo fainali ya UEFA.
Pia
walikosa kombe la mfalme ( copa de Rey) na sasa hawana matumaini ya kutwaa
ubingwa wa La Liga na kuwaachia kinyang`anyiro mahasimu wawili, Real Madrid na
Atletico Madrid.
Deco
aliyecheza Camp Nou kati ya mwaka 2004 na 2008 anadhani Barcelona
hawajachanganyikiwa na matokeo mabaya msimu huu, kwani wamekuwa wakionesha
juhudi kubwa hasa katika michezo mikubwa.
“Ni
ngumu kujua yanayoendelea Barca ukiwa nje. Watu wanasema mengi, lakini kwa
upande wangu kinachotokea ni kawaida katika michakato ya mpira”. Deco
ameliambia gazeti la Marca.
“Barca
wamepata makombe mengi miaka ya karibuni, wamekuwa katika kiwango cha
juu-walikuwa ni klabu bora zaidi duniani kwa mujibu wa watu wengi”.
“Kwa
kinachowatokeo sasa ni kawaida na wanapata uzoefu mzuri kuwa kwenye soka kuna
wakati mgumu pia”.
“Klabu
inatakiwa kujipanga upya kusaka mafanikio zaidi, iwabakishe nyota kama Lioel
Mess na Andres Iniesta ambao ni wachezaji muhimu kwa klabu”.
“Hakuna
haja ya kubadili mfumo wa uchezaji kwasababu ya matokeo mabaya”.
“
Tayari Barca wamekuwa na mpira wao na wanaweza kuuendeleza kama ilivyotokea
kipindi cha Louis van Gaal, Frank Rijkaard na Pep Guardiola walivyofanya”.
“Mfumo
wao ni kumiliki mpira na kwa hilo wao ndio bora zaidi duniani”. Alisema Deco.
Nyota
huyo wa kimataifa wa Ureno alikiri hakushangaa kuona Barcelona wanatolewa hatua
ya robo fainali msimu huu, lakini alishangazwa kuona Atletico Madrid wakiwatoa
Wakalunya.
“Ilinishitua
kwa Barca kundolewa UEFA. Kwa upande wangu niliwapa kura ya kutwaa ubingwa”.
Deco alisema.
“Lakini
sikushangazwa na waliowatoa Barca: Atletico. Wamekuwa na kitu cha ziada msimu
huu, huo ndio ukweli”.
Baada
ya kuwafunga Barca hatua ya robo fainali, Atletioc waliwatoa Chelsea jumatano ya
wiki hii na watakutana fainali na Real Madrid mei 24 mwaka huu mjini Lisbon,
Ureno.
0 comments:
Post a Comment