KOCHA wa Borrusia Dortmund, Jurgen Klopp
amesisitiza kuwa Bayern Munich bado ni klabu bora kuliko zote duniani licha ya
kutupwa nje hatua ya nusu fainali ya UEFA na Real Madrid.
The Bavarians ambao waliwafunga Dortmund katika
fainali ya UEFA mwaka jana uwanja wa Wembley, wameshindwa kutetea ubingwa wao
baada ya kupoteza mechi mbili kwa wastani wa mabao 5-0 na Los Blancos (Real
Madrid), kufuatia kufungwa mabao 4-0 katika mchezo wa marudiano Allianz Arena.
Klopp amejenga hoja yake kuwa japokuwa Madrid
wamedhihirisha kuwa Bayern wanafungika, lakini bado vijana wa Pep Guardiola
wanabaki kuwa klabu ya kwanza kwa ubora kwenye sayari hii ya tatu, (dunia).
“Bayern hawakulinda vizuri eneo leo dhidi ya Real
Madrid. Kwa upande wangu bado ndio klabu bora duniani, lakini wanaweza
kufungika”. Klopp amewaambia waandishi wa habari leo hii.
Klopp kwa sasa atamtumia mshambuliaji wake,
Mpoland, Robert Lewandowski katika mechi tatu kabla ya kujiunga na Bayern
kufuatia mkataba wake na Dortmund kumalizika majira ya kiangazi mwaka huu.
Klopp aliongeza kuwa : “Lewandowski amekuwa
mashambuliaji wa aina yake kwetu na tumefurahi kuwa naye muda wote. Natumaini
atafanya kazi nzuri katika mechi tatu alizosaliwa nazo”.
Dortmaund wanakutana na Hoffenheim katika mchezo
wao wa mwisho nyumbani Signal Iduna Park kabla ya kusafiri katika mechi moja ya
mwisho ya Bundesliga na kumalizia na fainali ya DFB Pokal dhidi ya Bayern
Munich ambayo itachezwa katika uwanja wa Olympiastadion.
Klopp,amekataa kuzungumzia sana mchezo wa
wikiendi.
“Ni mchezo wetu wa mwisho nyumbani msimu huu kabla
ya kwenda Berlin mara mbili na tunahitaji kuufurahia kwa njia sahihi. Alieleza kocha
huyo mwenye miaka 45.
“Roberto Firmino amerudi katika hali yake ya
kawaida kama ilivyo kwa Kevin Volland. Tutajilinda vizuri na tutapapa nafasi za
kufunga”.
"Marcel Schmelzer na Erik Durm tunatarajia
kuwa nao katika mechi hiyo.” Alihitimisha Klopp.
0 comments:
Post a Comment