

Balaa!: Suarez anapigana vilivyo na majeruhi ya goti lake ili acheze kombe la dunia baada ya kufanyiwa upasuaji jumanne ya wiki iliyopita.


Imechapishwa Mei 27, 2014, saa 9:34 asubuhi
LUIS
Suarez amemwambia mchezaji mwenzake wa Liverpool kuwa ana mpango wa
kubakia klabuni hapo msimu ujao ili kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa
wa ligi kuu soka nchini England.
Jana
jumatatu, Liverpool walisema kuwa kocha mkuu Brendan Rodgers amesaini
mkataba mpya utakaomuweka Anfield mpaka mwaka 2018 na atapata nguvu
zaidi kwa uwepo wa Suarez.
Ripoti
zinasema Real Madrid wameweka dau la paundi milioni 100 kwa ajili ya
kuinasa saini ya Suarez ambaye alisaini mkataba mrefu na Liverpool mwezi
desemba mwaka jana na aliahidi kukaa muda mrefu klabuni hapo.
Lakini vyanzo vya habari Bernabeu vinaeleza kuwa hakutakuwa na haja ya kumsajili Suarez kama Karim Benzema atakubali kusaini mkataba mpya.
Mfaransa huyo ambaye yuko kwenye rada za Arsenal anahitaji kuongezewa dau na Real Madrid, lakini klabu hiyo inaamini watafikia makubaliano na nyota huyo mwenye miaka 26 kabla ya kombe la dunia.
0 comments:
Post a Comment