

Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi
(kulia) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga mkataba wa
makabaliano yao kuhusu kuanzishwa kwa akaunti ya mashabiki na wanachama
wa klabu hiyo katika hafla iliyofanyika Hyatt Regency jijini Dar es
Salaam leo.
Viongozi
wa klabu za Simba na Yanga pamoja na viongozi Benki ya Posta Tanzania
(TPB) wakipozi kwa picha ya pomaja na Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia katika hafla ya uzinduzi wa akaunti ya
mashabiki na wanachama wa klabu hizo iliyofanyika Hyatt Regency jijini
Dar es Salaam leo.
Kutoka
kushoto, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, Naibu Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia, Ofisa Mtendaji Mkuu
wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi na Mwenyekiti wa
Simba, Ismail Aden Rage wakionyesha ishara ya kuendeleza soka katika
hafla ya uzinduzi wa akaunti maalum kwa ajili ya mashabiki na wanachama
wa klabu hizo iliyofanyika Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo.


0 comments:
Post a Comment