
HATIMAYE `deal done!`. Klabu ya Manchester United amemteua Louis van Gaal kuwa kocha mkuu mpya kufuatia kufukuzwa kazi kwa David Moyes mwezi uliopita.
Mholanzi huyo amechukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa muda wa Man United, Ryan Giggs aliyeteuliwa kuwa kocha msaidizi.
Frans
Hoek na Marcel Bout wajajiunga na Van Gaal kama makocha wasaidizi na
mholanzi huyo anakuwa kocha wa kwanza kutoka nje kuiongoza Man United.
Van
Gaal ataanza kazi rasmi baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la
dunia mwaka huu nchini Brazil ambako anaiongoza Uholanzi akiwa kocha
mkuu.

Van Gaal
akiwa na furaha amesema: 'Siku zote nilikuwa natamani kufanya kazi ligi kuu ya England. Kuwa kocha Manchester United, klabu kubwa duniani, inanifanya nijivune".
"Niliwahi kucheza mechi Od Traffford kabla na najua namna uwanja huu ulivyo na hamasa. Mashabiki wanapenda mno mpira. Klabu ina maono ya mbali; nami pia nina maono makubwa. Kwa pamoja nadhani tutaweka historia.".
Ryan Giggs alisema: "Nimefurahi kupata fursa ya kuwa kocha msaidizi. Van Gaal ni kocha bora duniani na najua nitajifunza vitu vingi kutoka kwake na kuchangia kadri niwezavyo".
"Manchester United ni sehemu ya maisha yangu kwa muda mrefu na nimefurahi kuendelea kuwepo na kufanya kazi muhimu kama hii".
Sehemu ya taarifa ya Manchester United inasomeka: "Louis van Gaal ataanza kazi ya ukocha mkuu wa Manchester United kuanzia msimu wa 2014/2015. Amesaini mkataba wa miaka mitatu".
0 comments:
Post a Comment