
Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars
imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa hatua inayofuata kuwania nafasi
ya kufuzu kwa fainali za kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, nchini,
Morocco. Stars iliichapa,timu ya Taifa ya Zimbabwe ' The Warrios' kwa goli 1-0,
siku ya jana katika mchezo wa kwanza wa mashindano kwa kocha mpya wa kikosi hicho,
Muholanzi, Martin Nooij.
Goli la dakika ya 13 lililofungwa na mshambulizi wa
kati, John Bocco lilifanya kikosi hicho kinachowania kufuzu kwa mara ya kwanza
fainali za Afrika tangu mwaka 1980 kuhitaji sare ya aina yoyote ili kusogea katika
hatua ya makundi. Mara ya mwisho, Stars ilifuzu kwa fainali za Afrika miaka 34
iliyopita nchini, Nigeria ikiwa na kikosi kilichoongozwa na rais aliyepita wa Shirikisho
la soka nchini, TFF, Ndugu, LeodgarTenga, Mtemi Ramadhani, meneja wa muda mrefu
wa timu hiyo , Leopard Tasso Mukebezi na nyota wengi wa soka la Tanzania wakati
huo.
Katika mchezo wa jana, kocha, Nooij aliwaanzisha washambuliaji
watatu, Bocco, ambaye alikuwa akizungukwa naThomas Ulimwengu aliyekuwa akishambulia
akitokea upande wa kulia, na Mbwana Samatta. Na wote watatu walihusika kwa goli
pekee lililopatikana ambalo litaipeleka timu, National Sports Stadium, Harare
ikiwa inajiamini.Samatta alitoa pasi ya kichwa kwa Ulimwengu ambaye alipiga pasi
safi ya mwisho kwa mfungaji, Bocco ambaye aliachia ' kiki kali' ya karibu.
Ilikuwa ni goli ' bab-kubwa' ambalo lilipangwa na wachezaji wenyewe.
Kwa muda mrefu, Stars imekuwa ikiangushwa na wachezaji
wa kikosi cha kwanza kushindwa kudumu katika viwango vyao wanapokuwa klabuni na
kufanya timu hiyo kuwa na mabadiliko kila wakati.Ila,namtazama kocha, Nooij na kumuona
mwenye bahati kubwa kuwa na wachezaji ambao walifanya kazi na makocha waliopita,
Marcio Maximo, Jan Poulsenna Kim Poulsen. Samatta na Ulimwengu wamekuwa wakicheza
nje ya Tanzania kwa miaka mitatu tena katika klabu bora barani Afrika, japo walikuwa
na uchovu wa kuiwakilisha, TP Mazembe katika michuano ya ligi ya mabingwa, siku
ya ijumaa iliyopita, wawili hao wanaweza kumsaidia, Nooij katika mipango yake.
Itapendeza kama, Bocco ataendelea kuwa katika kiwango
chake cha sasa kwa muda mrefu ujao, kwani itaifanya timu hiyo kuwa na uhakika wa
kufunga magoli, mshambulizi huyo wa klabu ya Azam FC,anashabaha akiwa klabuni kwake
lakini alikuwa akishindwa kujiamini anapokuwa Stars. Kwa miaka minne sasa yupo,
Stars hivyo anatakiwa kujiamini na kuhimili presha ya mashabiki kila anapokuwa akipoteza
nafasi.
Kwa namna mchezo wa jana ulivyokuwa, Stars iliundwa na wachezaji 10 kati ya 11 walioanza mchezo ambao tayari wamekuwa katika timu hiyo kwa miaka mitatu na kuendelea, kiungo Frank Domayo ana miaka miwili katika kikosi hicho na tangu alipoingia kwa mara ya kwanza, mwaka 2012 amekuwa ni mchezaji wa kikosi cha kwanza. Hakuwa katika kiwango chake cha kawaida katika mchezo jana, alipoteza mipira mingi,hakuwa akiisogeza timu mbele, na pasi zake nyingi hazikufika.Ila, bado ni mchezaji anayebeba matumaini ya muda mrefu katika safu ya kiungoya Stars kwani ndio kwanza anakaribia miaka 21. Akishirikiana na Mwinyi Kazimoto, pamoja na Mrisho Ngassa, safu ya kiungo ya Stars ilionekana kupotea wakati Fulani uwanjani na kuwafanya, viungo wa Zimbabwe, Rendai Ndoro, Milton Nauba,Kudakwashe Mahadina Cuthbert Malajila kutengeneza zaidi nafasi tatu katika uwanja wa ugenini.
Ushindi wa goli moja ni ' kiduchu ' lakini unatosha
kupunguza presha. Kufunga goli moja ugenini itakuwa ni sawa na kuwapa mlima mrefu
zaidi wapinzani kuupanda.Ila, wakati kocha wa ' The Warrios', Ian Gorowa akisema
timu yake ilikosa bahati ya kushinda japo walifanikiwa kutengeneza nafasi za kutosha,
Yule wa Stars, Nooij yeye kwa upande wake amesema kuwa timu yake ilicheza vizuri
na walishindwa kupata magoli ya kutosha kutokana na wachezaji kupoteza nafasi nyingi
walizotengeneza.
Zimbabwe inahitaji ushindi wa magoli 2-0 na kuendelea
ili wasonge mbele. Miaka miwili iliyopita, Stars ilitoka sare na Msumbiji katika
mchezo wa nyumbani na wakalazimisha sare ugenini ila wakatolewa na kwa mikwaju ya
penalty na kuondolewa katika harakati za kufuzu AFCON 2013.Wachezaji kadhaa bado
wapo kikosini, akiwamo Samatta aliyekosa mkwaju wa penalti( wakati huo ) hivyo tayari
wanao uzoefu wa michezo kama hiyo. Safu ya ulinzi ilicheza vizuri, japokuwa kuna
matatizo katika baadhi ya maeneo. Nadir Haroub na patna wake, Kelvin Yondan waliweza
kwenda sambamba na washambuliaji, Peter Moyona Eric Chipata.
Zimbamwe iliyokuwa bila wachezaji wake watatu wanaocheza
katika klabu ya Kaizer Chiefs ya AfrikaKusini, washambuliaji, Knowledge Musona
Knowledge na Kingston Nkhatha , pamoja na
kiungo mchezeshaji anayecheza pia katika klabu hiyo, Willard Katsande .Hivyo kocha
wa Stars anatakiwa kutazama namna walinzi wake wapembeni walivyokuwa rahisi kupitika
hasa kwa Shomari Kapombe aliyecheza kama mlinzi wa kulia. Oscar Joshua alikuwa
akiichezea Stars mchezo wake wa kwanza wa mashindano, hakupanda sana na hilo lilisaidia
safu nzima ya nyuma kutulia . Kama, Oscar angepotea zaidi kama ilivyokuwa kwa Kapombe
katika kipindi cha kwanza, Stars ingekuwa na wakati mgumu zaidi. Ila utulivu umefanya
timu kuwa na faida ya goli moja huku ikiwa haijaruhusu goli katika uwanja wa nyumbani.
Hii, siyo timu mpya, Ni timu ya muda mrefu ambayo kwa
kiasi Fulani imekomaa kama wachezaji watafanya mambo yao kwa uhakika kama ilivyokuwa
katika mchezo uliopita. Nooij, aliamua kuwaanzisha wachezaji wanne kati ya watano
wa klabu ya Yanga katika safu ya ulinzi na mpango huo ulitimia kwa kuwa,
Kapombe aliweza kwenda sambamba na Oscar katika kipindi cha pili, huku Nahodha,
Nadir na Yondan wakitimiza majukumu yao kama wachezaji wazoefu zaidi katika kikosi
hicho ambao tayari wamefanya kazi na Maximo, Jan na KIM.
Stars imeweka mguu mmoja ndani, ila ni muhimu wachezaji
kwenda ugenini kucheza zaidi ya walivyocheza katika mchezo wa kwanza. Goli moja
itamaanisha kuwa wenyeji watahitaji kufunga magoli zaidi ya matatu ili wafuzu kwa
hatua ijayo, ila tusisahau kuwa mechi inaweza kufika hadi hatua ya mikwaju ya
penalty. Mechi ya kwanza ya Mwalimu, Martin Nooij, Stars imekuwa ni nzuri kimatokeo
na kichezaji.
0714 08 43 08
0 comments:
Post a Comment