![]() |
Zamalek walishinda jana |
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 25, 2014, saa 5:32 asubuhi
LIGI ya mabingwa barani Afrika hatua ya
makundi iliendelea jana kwa mechi mbili kupigwa katika nchi mbili tofauti.
Al Ahly Benghazi ya Libya ikiwa
nyumbani iliibuka na ushindi mabao 3-2 dhidi ya Esperance ya Tunia.
Mchezo mwingine ulipigwa nchini Misri
ambao wenyeji Zamalek waliichapa Al Hilal ya Sudan mabao 2-1.
Ligi hiyo itaandelea leo kwa mechi
mbili kupigwa katika nchi mbili tofauti.
Nchini DR Congo, washambuliaji wa
kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samata na Thomas Emmanuel Ulimwengu
wataiongoza TP Mazembe mjini Lubumbashi kuwakabili mahasimu wao wa jadi, AS
Vita ya DR Congo.
Hii ni mechi inayovuta hisia za
mashabiki wengi barani Afrika kutokana na upinzani unaokuwepo mara timu hizi
zinapokutana, iwe katika ligi ya ndani au mashindano ya kimataifa.
![]() |
Majembe: Kila la heri vijana wetu Samata na Ulimwengu katika mchezo wa leo. |
Wiki za karibuni, TP Mazembe na AS Vita
walikutana katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya DR Congo mjini Kinshasa na
vijana wa Moise Katumbi kuibuka na ushindi wa bao1-0.
Hata hivyo mchezo huo uliingia katika
historia mbaya baada ya kutokea vurugu kubwa za mashabiki na kusababisha vifo
vya mashabiki zaidi ya 15.
Hakika tukio hili lilikuwa baya katika
ulimwengu wa soka, lakini chanzo chake ni mashabiki wa AS Vita kukosa uungwana
na kushindwa kukubali matokea.
Hofu imetanda mjini Lubumbashi
kwasababu siku za nyuma iliripotiwa kuwa mashabiki wa Mazembe wanaweza kulipa
kisasi kwa kile walichofanyiwa mjini Kinshasa.
Lakini taarifa kutoka nchini Congo
zinaeleza kuwa usalama utaimarishwa wakati wote wa mchezo na kwa bahati nzuri
hakuna rekodi ya vurugu katika uwanja wa Mazembe kama ilivyo kwa AS vita.
Wadau wa michezo wanaombea amani katika
mchezo huo na Mazembe wasilipize kisasa kwa AS Vita.
Mechi nyingine itapigwa nchini Algeria
ambapo wenyeji ES Setif watakabiliana na SC Sfaxien kutoka nchini Tunisia.
MSIMAMO WA MAKUNDI
MSIMAMO WA MAKUNDI
CAF Champions League | LOGS
Group A
Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | AS Vita (Congo DR) | 1 | 1 | 0 | 0 | 2 | 1 | 1 | 3 |
2 | Zamalek (Egypt) | 2 | 1 | 0 | 1 | 3 | 3 | 0 | 3 |
3 | Al Hilal (Sudan) | 2 | 1 | 0 | 1 | 2 | 2 | 0 | 3 |
4 | TP Mazembe (Congo DR) | 1 | 0 | 0 | 1 | 0 | 1 | -1 | 0 |
Group B
Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | CS Sfaxien (Tunisia) | 1 | 1 | 0 | 0 | 3 | 1 | 2 | 3 |
2 | ES Setif (Algeria) | 1 | 1 | 0 | 0 | 2 | 1 | 1 | 3 |
3 | Al Ahly Benghazi (Libya) | 2 | 1 | 0 | 1 | 4 | 5 | -1 | 3 |
4 | Esperance (Tunisia) | 2 | 0 | 0 | 2 | 3 | 5 | -2 | 0 |
0 comments:
Post a Comment