Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 25, 2014, saa 6: 03 mchana
WAGONGA Nyundo wa jijini Mbeya, Mbeya City fc jana walitoka nyuma na kushinda mabao 3-2 dhidi ya Academie Tchite ya Burundi katika mchezo wa kundi B wa michuano ya CECAFA Nile Basin Cup inayoendelea mjini Khartoum nchini Sudan.
Mbeya City fc waliofika Khartoum siku moja kabla
ya mechi walianza kufungwa bao katika dakika ya 10 baada ya Rashid kumtungua
kipa wao, lakini walirudi mchezoni baada ya Paul Nonga kusawazisha bao hilo
dakika 5 baadaye.
Dakika ya 27, nahodha wa Mbeya City fc, Mwegane
Yeya kama ilivyo kawaida yake alifunga bao la pili kwa njia ya kichwa. Them
Felix `Mnyama` alihitimisha karamu ya mabao dakika ya 37 baada ya kufunga bao
safi na kuwapeleka Mbeya City mapumziko wakiwa na furaha.
Kipindi cha pili, Waburundi walikuja na Presha
kubwa na katika dakika ya 68 Manirakiza alifunga bao la pili.
Kocha wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi aliwapongeza
vijana wake kwa ushindi na kuahidi kufanya vizuri mchezo unafuata.
"Vijana walipunguza kasi kipindi cha pili,
lakini nawasifu kwa kuvuna pointi tatu muhimu". Alisema Mwambusi.
Mpinzani wake, Ndayizeye Jimmy
aliwapongeza Mbeya City kwa soka safi.
Mbeya City: (Nonga paul-15’, Mwagane Yeya 27’
and Themy Felix 37’).
Mchezo mwingine ulipigwa kuanzia majira ya saa
2:00 usiku na kushuhudia AFC Leopard ya Kenya ikiibuka na ushindi mabao 2-0
dhidi ya Etincelles.
0 comments:
Post a Comment