
Na Mwandishi Wetu, Tanga
MABINGWA
wa Kombe la Uhai ambalo hushirikisha wachezaji wanaotumikia vikosi vya
pili kwenye timu zinazoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara,Coastal Union
U-20 Jumapili wiki hii wanatarajiwa kufanya ziara ya kimichezo Tarafa
ya Maramba wilayani Mkinga .
Timu
hiyo itacheza mchezo mmoja wa kirafiki na Viva Dynamo ya Maramba lengo
likiwa kujenga undugu na kuwapa burudani wapenzi wa soka wilaya pamoja
na kuwapa fursa kuiona timu hiyo ikicheza kwenye viwanja vyao vya
nyumbani.
Mchezo
huo unatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa soka JKT Maramba unaomilikiwa
na Jeshi la Kujenga Taifa wilayani humo ambapo msafara huo utaongozwa
na mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Hemed Aurora wakiwemo viongozi
wengine.
Akizungumza
na waandishi wa habari ,Ofisa Habari wa timu ya Coastal Union,Oscar
Assenga alisema ziara hiyo ni miongoni mwa mikakati ya timu hiyo
kuzunguka wilaya zote za mkoa wa Tanga kwa ajili ya maandalizi ya msimu
mpya wa Ligi kuu pamoja na mashindano ya Rolling Stone ambayo hufanyika
kila mwaka.
0 comments:
Post a Comment