
KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers
amefurahia kujipima uwezo na moja ya makocha wakubwa duniani, Louis van Gaal
anayetarajia kuiongoza Manchester United msimu ujao.
Mholanzi huyo alitangazwa kurithi
mikoba ya David Moyes jumatatu ya wiki hii kwa lengo la kurudisha hadhi ya Man
United, na kocha Rodgers anaona ni chaguo sahihi kwa mashetani wekundu.
Rodgers amemfurahia Van Gaal, lakini
amesema Moyes hakupewa muda zaidi wa kufanya makubwa Old Trafford.
“Kwanza kabisa, ilihuzunisha kuona
Moyes hakupewa fursa ya kutosha,”. Kocha huyo wa Liverpool aliwaambia talkSPORT.
![]() |
| Van Gaal |
“Moyes aliondoka na kwa vyovyote
vile walihitaji kutafuta kocha mwingine na wameona Van Gaal anastahili. Hata
mimi nakubali, ni mtu niliyejifunza kutoka kwake kwa miaka mingi”. Alisema
Rodgers.
“Ana
mafanikio makubwa, ni mtu mwenye maono makubwa na ana njia zake za kuona
mpira unachezwa. Anafanya kazi na wachezaji vijana. Nadhani ataifaa Manchester
United”.
“Nikiwa kocha kijana, nafurahi sana kushindana
na kocha mkubwa katika ulimwengu wa soka”.


0 comments:
Post a Comment