
NYOTA
wa zamani wa kimataifa wa Ureno, Luis Figo amesema Hispania haitabeba kombe la
dunia mwaka huu.
Figo
aliyeichezea Ureno mechi 125 na kufunga zaidi ya magoli 30 amesema kikosi cha
Vicente del Bosque hakina ubora wa kutetea ubingwa wao.
Hispania
imeshinda makombe makubwa matatu mfululizo kati ya mwaka 2008 na 2012, japokuwa
walipigwa na Brazil kwenye mechi Confederation Cup mwaka jana.
“Sidhani
kama Hispania watashinda kombe,” Figo aliuambai mtandao wa Laureus.com. “
Sidhani kama wana ubora wa kufanya hivyo. Itakuwa vigumu kwao kushinda, lakini
sio kwamba haiwezekani”.
Badala
yake Figo amewapa nafasi Brazil kutwaa ubingwa mwaka huu kwasababu wana kocha
bora na faida ya kucheza nyumbani.
“Nadhani
inasaidia kucheza nyumbani. Namjua vizuri kocha wa Brazil (Luis Felipe Scolari)
na naamini ni kocha bora kwa mashindano kama haya na nchi itaisaidia timu yao”.
Aliongeza Figo.
“Itakuwa
ngumu sana kwa timu zitakazocheza na Brazil ( kwasababu ya sapoti).”


Kiungo
huyo mstaafu alisema timu yake ya Ureno itahangaika sana kufika hatua za juu za
mashindano kwasababu inamtegemea zaidi Cristiano Ronaldo.

0 comments:
Post a Comment