
Anaondoka zake: Ronaldinho anapangisha nyumba yake mjini Rio baada ya kuachwa katika kikosi cha kombe la dunia.
Imechapishwa Mei 24, 2014, saa 1: 19 mchana
BAADA ya kuachwa katika
kikosi cha Luiz Felipe Scolari kitakachoshiriki kombe la dunia katika
ardhi ya nyumbani,
Ronaldinho `Gaucho` amebuni njia mpya ya kuingiza mkwanja kwenye
mashindano ya kombe la dunia yanayoanza majira ya kiangazi mwaka huu.
Mshambuliaji
huyo wa zamani wa Barcelona ameamua kupangisha nyumba yake iliyopo
mjini Rio de Janeiro kwa kodi ya Euro 9, 120 kwa usiku mmoja, lengo
likiwa ni kuwapa mashabiki fursa ya kula bata kwenye mjengo wa gwiji
huyo wa Brazil.
Ronaldinho
aliandika katika mtandao wake wa Twita kuthibitisha kuwa nyumba yake
yenye vyemba vitano ipo tayari kwa ajili ya kupangishwa wakati wa
mashindano na kama mtu anahitaji anatakiwa kufanya `mambo` kupitia
tovuti ya Airbnb.com.

Mandhari safi: Ronaldinho anapangisha nyumba yake ya vyumba vitano kwa kodi ya zaidi ya Euro 9,000 kwa usiku mmoja.

Kumbukumbu: Hapa ni wakati nyumba ya Ronaldinho inapakwa rangi enzi hizo akiwa AC Milan

Raha tupu: watu wana fursa ya kulala kwenye kitanda cha nyota huyo wa Brazil


Ronaldinho aliweka picha hii kwenye mtandao wa Twita iliyochukuliwa akiwa nyumbani kwake

Tayari kwa raha: Chumba kikubwa cha kulia chakula kinaweza kuchukua wageni 10

Kupiga mbizi kupo kama kawaida: Nyumba ya Ronaldinho ina mabwawa safi ya kuogelea.
0 comments:
Post a Comment