


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 31, 2014, saa 10: 12 jioni
WENYEJI wa michuano ya CECAFA
Nile Basin Cup, Al-Merreikh ya Sudan wametupwa nje ya michuano hiyo kwa
penati 3-2 baada ya dakika 90 za kawaida kumalizika kwa sare ya bao 1-1
dhidi ya Academie Tchite ya Burundi.
Merreikh ndio walikuwa wa kwanza
kuandika bao la kuongoza dakika ya 4 kupitia kwa Agab Ramadan, lakini
dakika ya 22 Academie wakasawazisha kupitia kwa Manishimwe Alain na
matokeo hayo yalidumu mpaka dakika ya 90 na mshindi kupatikana kwa
mikwaju ya penati.
Wachezaji wa Al-Merreikh waliokosa penati ni Amir Kamal, Wawa Pascal na
Tia Togbi Olivier. Waliofunga ni Only Sadjo Haman na Elbasha Ahmed.
Vijana wa Academie waliofunga
penati jana ni Ngando Omar, Barampanze Shaban na Manishimwe Alain.
Mlinda mlango wa Academie Sonzera Anslem ndiye alikuwa nyota wa mchezo
huo.
Mchezo wa mapema wa robo fainali uliwakutanisha AFC Leopard ya Kenya na Defence kutoka nchini Ethiopia.
Mchezo huo ulimalizika kwa
Leopard kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 na kuandika historia ya kuwa
timu ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hii mipya katika
ukanda huu wa Afrika mashariki.
Kamati ya mashindano ya CECAFA
Nile Basin Cup imekutana leo asubuhi katika Hoteli ya Grand Holiday
Villa mjini Khartoum, imehamishia mechi zote kwenda uwanja wa Khartoum.
Mechi za leo za robo fainali kati
ya Victoria University dhidi ya Mbeya City fc na nyingine ya
Ahly-Shandy na Malakia fc zilipangwa kufanyika kwenye uwanja wa
Al-Merreikh.
Lakini barua iliyotumwa kwa klabu
zote na katibu mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye anasema mabadiliko hayo
yanatakiwa kufanyiwa kazi mara moja.
“Kutokana na majukumu mengine ya
uwanja wa Al-Merreikh, ninataarifu kuwa mechi zote zilizosalia leo
jumamosi, zimehamishiwa uwanja wa Khartoum. Tunaomba radhi kwa usumbufu
wowote uliojitokeza”. Ilisomeka barua ya Musonye.
0 comments:
Post a Comment