
Muda
 mchache baada ya klabu ya Manchester United kuthibitisha kumtimua kazi 
kocha David Moyes, shirika la utangazaji wa Uingereza BBC limetangaza 
kwamba makocha wasaidizi wa Moyes, Steve Round na Jimmy Lumsden nao 
wameondolewa kwenye vibarua vyao.
Wakati huo huo imethibitishwa kwamba Ryan Giggs na Nicky Butt wataiongoza timu hiyo katika michezo minne iliyobakia.
Hata hivyo mpaka sasa majina ya kocha Uholanzi  Louis Van Gaal, wa 
Borussia Dortmund Jurgen Klopp, Atletico Madrid’s manager Diego Simeone 
na Ryan Giggs wanatajwa kuewa nafasi ya kuifundisha timu hiyo kuanzia 
msimu ujao.




0 comments:
Post a Comment