
Jürgen Klopp
 amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kuteuliwa nafasi ya ukocha wa 
klabu ya Manchester United. Kocha huyo mwenye miaka 46 ameliambia gazeti
 la The Guardian la Uingereza: “Man Utd ni klabu kubwa na nahisi kuwa 
mazingira yake nina uzoefu nayo na ina mashabiki wazuri sana, lakini 
mpaka sasa nina mkataba na Dortmund na imani yangu kwa mashabiki wa 
klabu hiyo haiwezi kuvunjwa.”
Klopp, ambaye anatajwa kuwa na kipenzi kikubwa cha bodi ya 
wakurugenzi ya Manchester United, aliongeza mkataba wake na Dortmund 
mpaka 2018 mwaka jana Oktoba na alikaririwa akisema kwamba bado 
anaipenda klabu hiyo wiki iliyopita. Inaaminika United walijaribu 
kufanya mazungumzo na Dortmund lakini walijibiwa kwamba Klopp hakuwa na 
nia ya kuvunja mkataba wake ndani ya Signal Iduna Park.




0 comments:
Post a Comment