Na
Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
TIMU
tatu mpya zitakazocheza ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 tayari zimeshajulikana
na kinachosubiriwa ni kupata timu tatu za kushuka daraja ili kuwapisha wageni.
Watu
wa Shinyanga msimu ujao watafaidi uhondo wa wa ligi kuu baada ya vijana wao wa
Stand United kupanda daraja msimu huu.
Nao
wazee wa Ndanda fc kwa `roho safi` kutoka mkoani Mtwara watafurahia mitanange ya
ligi kuu baada ya timu yao kupanda daraja.
Timu
ya tatu ni Polisi Morogoro ambayo ilikuwepo msimu wa mwaka jana, lakini ilishuka
na kupanda msimu huu tena.
Wakati
wanashuka pamoja na Africa Lyon, na Toto Africans ya mwanza, Polisi Morogoro
waliahidi kurudi ndani ya mwaka mmoja na kweli wamefanikiwa.
Lyon
na Toto zimeshindwa kurudi ligi kuu kwasababu ya kushindwa kuhimili mikikimikiki
ya ligi daraja la kwanza msimu huu.
Wakati
timu hizi tatu zikishuka msimu wa mwaka jana, ziliwapisha Mbeya City,
Rhino Rangers, na Ashanti United.
Timu
tatu zilizopanda msimu huu, ni Mbeya City yenye uhakika wa kusalia ligi kuu kwa
asilimia 100.
Ashanti
United wapo katika hali ngumu zaidi ambapo wanachuana na Prisons, Mgambo JKT na
JKT Ruvu kukwepa kushuka daraja.
Rhino
Rangers tayari walishakata tiketi ya
kuporomoka daraja, huku nao JKT Oljoro wakionekana kuungana na safari hii
ya kushuka daraja. Hakuna miujiza juu ya hili.
Kinachosubiriwa
kwa hamu ni kuona kati ya timu mpya tatu
zilizopanda, nani atarithi mikoba ya Mbeya City, Rhino Rangers na Ashanti
United kwa maana ya ushindani ndani ya ligi kuu msimu huu.

Mbeya City fc wamewavutia watu wa Shinyanga na Mtwara, wamesema wataziunga timu zao kama watu wa Mbeya
Wadau
wa mikoa ambayo timu hizi tatu zimeshapanda ligi kuu wamekuwa wakisikika kuwa
wataziunga mkono timu zao kama wafanyavyo watu wa Mbeya.
Mbeya
city fc imejizolea umaarufu mkubwa na mashabiki lukuki, hivyo kuwa gumzo katika
klabu kubwa za Simba, Yanga na Azam fc.
Mpaka
sasa City ipo nafasi ta tatu kwa pointi
45, huku ikiwa na miwili mkononi.
Kwa
msimu wao wa kwanza, haya ni mafanikio makubwa sana na wakijipanga zaidi kwa
kuanzia watakapofikia msimu huu basi wanaweza kuwa timu bora na yenye ushindani
wa hali ya juu msimu ujao.
Imekuwa
jambo safi kusikia watu wa Mtwara na Shinyanga
wakiwa na mikakati ya kuzipiga chini Simba na Yanga na kurudisha
uzalendo kwa timu zao za nyumbani.
Kwa
hili Mbeya City fc lazima wapewe sifa zao kwasababu wamekuwa mfano kwa mikoa
hii na kama kweli wataweza kufanya kama watu wa Mbeya, basi tutegemee timu
nyingine bora kati ya Stand United na Ndanda fc ya Mtwara.
Watu
wa Mtwara wamefika mbali zaidi kwa kuanzisha falsafa yao ya Ndanda fc `kwa roho safi`,
wakimaanisha kila kitu ni timu yao, wengine pembeni.
Ni
vizuri kuwaiga Mbeya City fc, lakini stand United, Ndanda fc na Polisi Morogoro
wanatakiwa kuwa na mipango mizuri ili kufikia mafanikio ya Wagonga nyundo wa
Mbeya.
Kwanza
wahakikishe wanasajili vizuri kwa kutozingatia majina ya wachezaji.
Wakae
chini kusaka vijana wadogo wenye vipaji na wenye umri mdogo ambao wanaweza
kuwekwa pamoja na kufundishika kirahisi.
Waepukane
na siasa katika mpira, wawaache walimu wao wafanye kazi yao na watengeneze
mazingira mazuri kwa wachezaji wao kuanzia posho na mishahara.
Pia
wakae na wachezaji wao kuwapandikiza `Sumu` ya kuwa wazalendo na timu yao.
Wajiandae
kiuchumi ili waweza kusafiri na timu zao kwenda mikoani kama wafanyavyo watu wa
Mbeya City.
Wajejela Tanzania Prisons wanachuana na Ashanti United kukwepa kushuka daraja
Tayari
timu tatu zimeshapatikana, swali la msingi ni, je, timu gani tatu zinashuka
daraja kuzipisha timu hizi mpya?.
Mtandao
huu unafanya uchambuzi wa kina ili kuona ni timu gani zinashuka daraja.
Kwanza
tuangalie msimamo wa timu za mwisho
kuanzia nafasi ya 9 katika msimamo wa
ligi kuu Tanzania bara mpaka sasa.
Nafasi
ya 14 mkiani, Rhino Rangers wameshapiga kambi yao baada ya kucheza mechi 24 na
kujikusanyia pointi 16 tu.
Hata
hivyo maafande wa Rhino wamebakiza mechi mbili ambazo wakishinda watafikisha
pointi 22 pekee.
Nafasi
ya 13 wapo JKT Oljoro wenye pointi 18 baada ya kucheza mechi 24, huku
wakibakiwa na michezo miwili na kama watashinda yote watafikisha pointi 24.
Nafasi
ya 12 wapo Ashanti United wenye pointi 22 baada ya kucheza mechi 24. Wauza
mitumba hawa wa Ilala wamebakiza mechi mbili na kama watashinda zote
watafikisha pointi 28.
Nafasi
ya 11 wapo Tanzania Prisons wenye pointi 22 baada ya kushuka dimbani mara 24,
na kama watashinda mechi mbili zilizosalia watafikisha pointi 28 kama Ashanti
United.
Nafasi
ya 10 wapo Mgambo JKT wenye pointi 25 baada ya kucheza mechi 24. Na kama
watashinda mechi zao mbili zilizobaki wataweza kufikisga pointi 31.
JKT
Ruvu wapo nafasi ya 9 kwa pointi 28 baada ya kucheza mechi 24. Na kama
watashinda mechi zote mbili walizobakiza watafikisha pointi 34.
Ukipiga
hesabu, kama timu zote za mwisho zitashinda mechi zao, msimamo utakuwa hivi;
Maafande wa Rhino Rangers wameshashuka daraja kwa asilimia zote
JKT
Ruvu watakuwa nafasi ya 9 kwa pointi 34. Lakini itategemeana na matokeo ya Mtibwa Sugar na Coastal Union kwani
wataweza kuvuka pointi hizo kama wa watashinda mechi zao mbili za mwisho.
Coastal
wapo nafasi ya na 8 kwa pointi 29 baada ya kucheza mechi 24, hivyo wakishinda
michezo yake miwili watafikisha pointi 35.
Mtibwa
wapo nafasi ya 7 kwa pointi 30 baada ya kucheza mechi 24. Na kama watashinda
mechi mbili walizobakiza watafikisha pointi 36.
Na
ndio maana nafasi ya JKT Ruvu inaweza kuwa ya 9 mpaka mwisho wa msimu au ikawa
tofauti.
Nafasi
ya 10 Mgambo watakaa kwa pointi 31, huku nafasi ya 11 na 12 zikikaliwa na Prisons,
Ashanti watakaokuwa na pointi 28 kila mmoja, lakini utofauti wa mabao ya
kufunga na kufungwa yataweza kuwatofautisha.
Nafasi
ya 13 watakuwepo JKT Oljoro watakaokuwa na pointi 24, na Rhino Rangers wataburuza mkia kwa pointi 22.
Hivyo
ndivyo msimamo wa ligi kwa timu za mwisho utakavyokuwa kama timu zote
zitashinda mechi zao za mwisho.
Kwa
maana hiyo, Rhino Rangers watakaokuwa na pointi 22, JKT Oljoro pointi 24 na
mmoja kati ya Ashanti United na Prisons wataungana na timu hizi mbili kushuka
daraja kwa kuangalia wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Mgambo JKT wamekaza sana safari hii
Rhino
na Oljoro wana asilimia zote za kushuka daraja, lakini vita ya Ashanti na
Prisons haipimiki kabisa. Huku Mgambo akionekana kuimarika zaidi.
Wakati
tunatabiri matokeo hayo, lazima tufahamu timu hizi zimebakiwa na mechi za aina
gani.
Rhino
wamebakiza mechi dhidi ya Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine Mbeya na mchezo wa
mwisho watacheza na Ruvu Shooting uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
JKT
Oljoro wamebakiza mechi dhidi ya Yanga na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Shk.
Amri Abeid jijini Arusha.
Ashanti
wamebakiza mechi dhidi ya Simba sc uwanja wa Taifa pamoja na Tanzania Prisons
uwanja wa Sokoine Mbeya.
Prisons
wamebakiza mechi dhidi ya Rhino na Ashanti uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mgambo
JKT wataumana na Kagera Sugar Mkwakwani na mechi ya mwisho watacheza na Mbeya
City sokoine jijini Mbeya.
Ashanti United wapo katika hatari kubwa ya kushuka daraja
JKT
Ruvu wamebakiza mechi na coastal union Mkwakwani na mechi ya mwisho watacheza
na Azam fc uwanja wa Azam Complex.
Ukizipima
mechi hizi nje ya uwanja, utagundua kirahisi kuwa timu hizi hazina uwezo wa
kushinda mechi zote zilizobaki kirahisi.
Kwasababu
kuna baadhi ya mechi watacheza na timu zinazohitaji ubingwa kwa maana ya Yanga
na Azam fc.
Pia
nyingine kuna mechi dhidi ya Mbeya City wanaohitaji nafasi ya pili na tatu
msimu huu.
Kwa
maana hiyo mechi hizo zitakuwa ngumu zaidi kutokana na mazingira hayo ya Yanga,
Azam fc na Mbeya City.
Tusubiri kuona nani atashuka daraja na nani atatwaa ubingwa.
Lakini kwa ndugu zangu Oljoro na Rhino, kama wameshatoa mkono wa `bai bai` vile.
Prisons na Ashanti wanachuana vikali. JKT Ruvu na Mgambo JKT angalau wanapumua kwa kiasi fulani.
Azam fc wapo kileleni kwa pointi 53 na wapo katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa
Sijua kama watashangilia ubingwa wao kwa staili hii?
Kwa
ubingwa, Yanga na Azam fc ngoma bado nzito. Hawezi kutabiri kirahisi ingawa
Azam fc wapo mbele kwa pointi 4 na wameshafungana michezo 23 na Yanga.
Kama
Azam fc watashinda mechi mbili zilizobaki na kupoteza mechi moja, basi
watawavua rasmi ubingwa Yanga kwasababu watafikisha pointi 59 ambazo Yanga
hawataweza kufikia hata wakishinda mechi zote zilizosalia.
Kama
Yanga watashinda mechi zote basi watafikisha pointi 58 ambazo zitapitwa na Azam
fc.
Kibarua
cha ubingwa kinaanza kesho kutwa ambapo Yanga watakuwa na Kagera Sugar uwanja
wa Taifa , wakati Azam fc wakiwa na Ruvu Shooting Mabatini Mlandizi mkoani
Pwani.







0 comments:
Post a Comment