Kazini mapema: Ryan Giggs akiendesha kuelekea Uwanja wa mazoezi wa Manchester United, Carrington leo asubuhi
MKONGWE
 Ryan Giggs alionekana vizuri na aliye tayari kwa kazi Manchester United
 wakati anawasili kazini leo katika siku ya kwanza tangu kutangazwa kuwa
 mrithi wa muda wa David Moyes. 
Giggs
 amepewa ukocha wa muda wakati mchakato wa kumsaka kocha mpya 
unaendelea, kufuatia kuondoka kwa Moyes baada ya miezi 10 tu ya Mkataba 
wake wa miaka sita.  
Gwiji
 huyo wa Wales aliwasili katika Uwanja wa mazoezi wa klabu, Carrington 
Saa 2.10 leo asubuhi kabla ya Wayne Rooney, Rio Ferdinand, Michael 
Carrick na nyota wengine wa United kwa maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu 
England dhidi ya Norwich mwishoni mwa wiki.  
 
Wakati
 huo huo: Mkongwe mwingine wa timu hiyo, Paul Scholes alihudhuria 
programu kamili ya mazoezi leo Carrington baada ya kurejeshwa klabuni 
kama mmoja wa maofisa wa benchi la Ufundi.
Ilielezwa jana kwamba mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 39 atafanya kazi chini ya Ryan Giggs, aliyerithi mikoba ya David Moyes.

Amerudi:
 Paul Scholes akiwa na Wayne Rooney mazoezini enzi zake anacheza, leo 
amefika kama kocha baada ya kufukuzwa kwa David Moyes





0 comments:
Post a Comment