Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
0712461976 au 0764302956
SASA kimeeleweka Simba Sc na huenda kiu ya wanachama wake imekatwa baada ya kikao
cha Kamati ya Utendaji kilichomalizika
mchana wa leo jijini Dar es Salaam, kupanga Mei 4,mwaka huu iwe tarahe ya
Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo.
Afisa Habari wa Simba SC, Asha Muhaji ameuambia mtandao huu kuwa kikao hicho pia
kimeunda Kamati ya Uchaguzi.
Alisema Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ni
mwanasheria mashuhuri, Damas Ndumbaro na Makamu wake ni Salum Madenge.
Wajumbe wengine ni Issa Batenga ambaye ni Katibu,
Khalid Kamguna Katibu Msaidizi na Wajumbe Kassim Dewji, Juma Simba na Amin
Bakhresa.
Jambo lingine ambalo Asha alieleza ni kuwa kesho, Simba
SC inatarajiwa kufanya mkutano wa wanachama wake kwa ajili ya kuifanyia
marekebisho Katiba yao kwa maagizo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Afisa habari huyo aliwaomba wanachama hai wa klabu
hiyo kujitokeza kwa wingi zaidi katika mkutano huo muhimu kwa maandeleo ya
klabu.
Msikilize `Live` Asha Muhaji wakati akihojiwa na
mtandao huu jioni hii
Bofya hapa chini
0 comments:
Post a Comment