Vincent Kompany baada ya kuoneshwa kadi yekundu ya moja kwa moja katika mchezo wa leo
MANCHESTER City imerudi nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Hull City leo hii.
Timu ya Manuel Pellegrini leo ilijipanga kuvuna pointi tatu katika Ligi Kuu na shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, David Silva dakika ya 14 na Edin Dzeko dakika ya 90. Lakini City ilimaliza pungufu baada ya Nahodha wake, Vincent Kompany kutolewa nje kwa nyekundu dakika ya 10 baada ya kumchezea rafu mshambuliaji wa Hull City, Nikica Jelavic.
Kwa ushindi huo,City inatimiza pointi 60 baada ya kucheza mechi 27 na kurejea nafasi ya pili, nyuma ya Chelsea yenye pointi 66 baada ya mechi 29.
MATOKEO YA MECHI ZOTE HAYA HAPA, LAKINI MCHEZO WA CHELSEA UNAENDELEA
0 comments:
Post a Comment