Sunday, March 9, 2014

Na Baraka Mpenja , Dar es salaam

0712461976 au 0764302956

WEKUNDU  wa Msimbazi Simba wamelazimisha suluhu ya bila kufungana na Maafande wa Tanzania Prisons katika dimba la CCM Sokoine jijini Mbeya.

Simba waliingia uwanjani wakiwa na matumaini ya kuibuka na ushindi, lakini ugumu wa wajelajela mzunguko huu wa pili umewanyima ushindi vijana wa Dravko Logarusic.

Akizungumza kutoka Mbeya, afisa habari wa Simba, Asha Muhaji amesema kuwa mchezo ulikuwa mgumu sana kwao kulingana na mazingira ya wapinzani wao.

“Simba tunahitaji kufanya vizuri ili tukae nafasi nzuri katika msimamo, wakati Prisons wao wanahitaji pointi ili kuendelea kujinusuru kushuka daraja. Kwa mazingira hayo ndio maana mechi ilikuwa ngumu kwa timu zote”. Alisema Asha.

Aidha aliwaomba mashabiki wa Simba kuendelea kuiunga mkono klabu yao kwani bado wanazo mechi mkokoni na wanatarajia kufanya vizuri.

Kwa upande wao Tanzania Prisons kupitia kwa katibu mkuu wake, Sadick Jumbe walisema haikuwa rahisi kwa Simba kupata ushindi katika mchezo wa leo kutokana na ubora wao.

“Nilisema toka mchana kuwa Mnyama hawezi kutoka sokoine. Bahati nzuri wametoa suluhu. Sisi tumejipanga vizuri na leo hii tumevuna pointi moja na kufikisha 22, hakika tutabakika ligi kuu”. Alijisifu Jumbe.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 36 katika nafasi ya nne ya msimamo baada ya kucheza mechi 21.

Prisons wamefikisha pointi 22 baada ya kucheza mechi 20, lakini bado inasalia nafasi ya 10 katika msimamo.

Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Yaw Berko, Haruna Shamte, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Haroun Chanongo/Betram Mombeki dk46, Henry Joseph/Said Ndemla dk82, Amri Kiemba, Amisi Tambwe na Ramadhani Singano ‘Messi’/Ali Badru dk70.
Prisons; Beno Kakulanya, Salum Kimenya, Laurian Mpalile, Jumanne Fadhil, Lugano Mwangama, Nurdin Issa, Freddy Chudu, Omega Seme/Jimmy Shoji dk88, Peter Michael/Brighton Mponzi dk86, Frank Hau na Sixbert Mwasekaga.


Mchezo mwingine wa ligi kuu ulikuwa katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambapo JKT Ruvu wameshinda mabao 2-1 dhidi ya wana TamTam Mtibwa Sugar.

Mabao ya JKT Ruvu yamefungwa  na Hussein Bunu dakika ya 39 na Amos Mgisa dakika ya 75, wakati bao la Wakata Miwa wa Manungu lilifungwa na Vincent Barnabas dakika ya 70.

Akizungumza baada ya mechi, msemaji wa Mtibwa Sugar Tobias Kifaru Lugalambwike alikiri kuwa wapo katika wakati mgumu msimu huu kutokana na ushindani kuwa mkubwa.

“Tumefungwa leo hii. JKT Ruvu walicheza kwa kujituma. Wametumia nafasi walizopata, sisi tumetumia moja. Tunaangalia mbele”. Alisema Kifaru.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video