Wednesday, March 19, 2014

1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwan Kikwete wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Polisi mjini Chalinze leo ambapo amemuelezea Ridhiwani kama kijana aliyelelewa vyema na chama cha Mapinduzi na wananchi wa jimbo la Chalinze wamchague mgombea huyo kwani ataweza kuwawakilisha vyema bungeni na kutatua matatizo ya jimbo hilo kwakuwa yeye ni mwana CCM na ilani inayotekelezwa ni ya CCM, Uchaguzi wa jimbo la Chalinze unatarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE)2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa jimbo la Chalinze katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze leo.3Mgombea wa ubunge jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwan Kikwete akiwahutubia wananchi wa jimbo la Chalinze wakati alipokuwa akiomba kura.4Mama Salma Kikwete Mke wa Rais na mjumbe wa Halimashauri kuu kutoka mkoa wa Lindi akimsikiliza mmoja wa waliokuwa wagombea wa jimbo la Chalinze katika mchujo ndani ya Chama cha Mapinduzi Ndugu Imani Madega mara baada ya kumuombea kura Rihiwani Kikwete, katikati ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadik5mmoja wa waliokuwa wagombea wa jimbo la Chalinze katika mchujo ndani ya Chama cha Mapinduzi Ndugu Imani Madega kulia akizungumza na Ridhiwani Kikwete mara baada ya kumuombea kura6mmoja wa waliokuwa wagombea wa jimbo la Chalinze katika mchujo ndani ya Chama cha Mapinduzi Ndugu Imani Madega akimuombea kura Ridhiwani Kikwete.7Msaniki Sam wa Ukweli kushoto akiwa katika picha ya pamoja na mpenzi wa Chama cha Mapinduzi Bw. Mustafa Selemani.8Mama Salma Kikwete Mke wa Rais na mjumbe wa Halimashauri kuu kutoka mkoa wa Lindi akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.9Mbunge wa Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka akiwahutubia wananchi wa Chalinze wakati wa mkutano huo.10Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza na kukaribisha baadhi ya viongozi katika mkutano huo.11Mama Salma Kikwete Mke wa Rais na mjumbe wa Halimashauri kuu kutoka mkoa wa Lindi akimsikiliza mkuuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadik.13Kundi la muziki la TOT likitumbuiza katika mkutano huo.14Wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wakiwa wamebeba Picha za mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM Bw. Ridhiwani Kikwete.15Malkia wa muziki wa Taarab kutoka kundi la TOT Khadija Omar Kopa kulia akiongoza kundi hilo wakati lililpokuwa likitumbiza katika mkutano huo leo.16Marafiki mbalimbali wa mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM Bw. Ridhiwani Kikwete waliojitokeza katika mkutano huo  wakinyanyua juujuu mabango yenye picha zaRidhiwani Kikwete.17Cheki hili nyomi18Mama Salma Kikwete Mke wa Rais na mjumbe wa Halimashauri kuu kutoka mkoa wa Lindi kulia, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati na mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete wakiondoka eneo la Mkutano mara baada ya kumalizika.19Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati, Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi na Ridhiwani Kikwete wakitembea kwa miguu kuelekea eneo la mkutano uliofanyika viwanja vya Polizi mjini Chalinze leo.20Mama Salma Kikwete Mke wa Rais na mjumbe wa Halimashauri kuu kutoka mkoa wa Lindi kulia akiselebuka pamoja na akina mama wana CCM mara baada ya kuwasili katika mkutano huo.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video