Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
0712461976 au 0764302956
MECHI ya watani wa jadi wa kaskazini mwa London baina ya Asernal na Tottenham Hospur imemalizika Usiku huu kwa washika bunduki wa Aserne Wenger kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kurudi katika mbio za ubingwa wa ligi kuu soka nchini England.
Bao pekee la Tomas Rosicky katika sekunde ya 72 kipindi cha kwanza limewapa ushindi wa kwanza Asernal dhidi ya Tottenham katika dimba la White Hart Lane tangu mwaka 2007.
Kikosi cha Tim Sherwood kitajilaumu sana katika mchezo wa leo kwasababu kilitawala mchezo kwa dakika nyingi na kiungo wake Nacer Chadli alikosa bao la wazi la kusawazisha kufuatia makosa ya mlinda mlango wa Arsenal, Wojciech Szczesny.
Leo hii wenyeji walishindwa kufanya maajabu, na sasa kocha wa Asernal, Aserne Wenger anajiandaa kukabiliana na Chelsea wiki ijayo ambapo utakuwa mchezo wake wa 10,000 tangu awe kocha wa washika bunduki hao wa London.
Na Baada ya matokeo ya leo, Asernal imekuwa nyuma kwa pointi 4 tu dhidi ya vinara Chelsea, huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.



Mwokozi wa leo: Rosicky (katikati) akishangilia baada ya kufunga bao usiku huu katika dimba la White Hart Lane

Kikosi cha Tottenham leo: Lloris 6, Naughton 6, Kaboul 6, Vertonghen 6.5, Rose 5.5, Chadli 6 (Sigurdsson 69mins, 6), Sandro 5.5 (Paulinho 68mins, 6), Eriksen 6 (Soldado 82mins, 6), Bentaleb 5, Townsend 6, Adebayor 5.5
Wachezaji wa akiba: Friedel, Kane, Walker, Lennon
Waliooneshwa kadi za njano: Chadli, Sandro, Vertonghen, Soldado, Rose
Kocha: Tim Sherwood 5
Kikosi cha Arsenal: Szczesny 6.5, Sagna 6.5, Mertesacker 8, Koscielny 7, Gibbs 7, Rosicky 7.5 (Flamini 69mins, 6), Arteta 7, Oxlade-Chamberlain 7.5 (Vermaelen 85mins, 6), Cazorla 6, Podolski 6.5, (Monreal 77mins, 6), Giroud 5.5
Wachezaji wa akiba: Fabianski, Sanogo, Jenkinson, Gnabry
Waliooneshwa kadi za njano: Sagna, Gibbs, Flamini
Bao : Rosicky 2
Kocha: Arsene Wenger 7
Mchezaji bora wa mechi: Mertesacker
Mwamuzi: Mike Dean (Wirral)
0 comments:
Post a Comment