Na KIBADA Kibada Katavi
Wanaume
 Mkoani Katavi wamepewa changamoto kutoa taarifa  kwa jeshi la polisi 
wanapofanyiwa vitendo vya unyanyasaji  na wake  zao.
Changamoto
 hiyo ilitoewa hivi na Mkuu wa Kitengo Jeshi la polisi Mkoani Katavi  
kupitia kitengo  cha dawati la jinsia na unyanyasaji wa watoto sodoka 
vijinia Sodoka katika maazimisho ya siku kumi na sita ya kupinga 
unyanyasaji wa watoto na wanawake pia hata wanaume wananyanyaswa na wake
 zao majumbani na kukaa kimya bila kutoa taarifa kwa jeshi la polisi 
hivyo hakuna taarifa sahihi kuhusu hilo.
 Kutokana na changamoto hiyo    
jamii inatakiwa kuelewa na kufichua maovu ya unyanyasaji wanayofanyiwa 
watoto katika  Mkoa  wa Katavi.Amevitaja baadhi ya vitendo hivyo wanavyofanyiwa watoto na wanawake walio wengi majumbani kuwa ni kupigwa ,kuchomwa moto kunyimwa chakula.
Vitendo vingine ni pamoja na ubakaji ili kwa hali hiyo wasikae kimywa watoe taarifa polisi watasaidiwa na wataweza kufichuliwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
wiki ya unyanayasaji kinjisia ambapo wameazishwa kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo.
Bi 
Sodoka akiongea kwa nyakati tofauti katika wadi ya wazazi,wadi, ya 
wanaume na wadi ya watoto katika kauli zake  amewashauri wazazi 
kuhakikisha  watoto wanapofanyiwa vitendo vya  unyanyasaji kama kubakwa 
wapelekwe polisi ndani ya masaa 72 kabla ya kwenda Hospitali ili sheria 
iweze kuchukua mkondo wake wao polisi watatoa utaratibu wa kibali cha 
kwenda Hospitali kutibiwa na mhusika atachukuliwa hatua lakini kama 
hawatatoa ushirikiano hawatafahamu kinachoendelea.
Akizungumzia
 mahusiano ya Jeshi la polisi na jamii alisema wao ni sehemu ya jamii 
hivyo hawana budi kushirikiana kwa ukaribu na jamii wanayoishi nayo ili 
kudumisha amani na usalama katika jamii hiyo.
Kwa 
upande wake mmoja wa wauguzi aliyepokea zawadi kutoka kitengo cha dawati
 la jinsia Bi Lucy Baruti alifurahishwa na kitendo cha jeshi la polisi 
kuwathamini na kuja kuwaona wagonjwa kwa kuwaletea zawadi za sabuni, 
biskuti na  mafuta ambavyo vitasaidia kwa njia moja au nyingine 
kuwafariji wagonjwa.


0 comments:
Post a Comment