Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
Tel: 0712461976 au 0764302956
BAADA ya kutolewa katika mchezo wa nusu fainali wa klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA, inawezekana Ronaldinho alikuwa anataka kurejea kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha klabu yake ya Atletico Mineiro ili kujiliwaza kufuatia kula kipigo.
Lakini mambo yalikuwa tofauti baada ya kujikuta akikaa uwanjani kutokana na wachezaji wa Casablanca kumvamia wakiomba viatu vyake vya Nike.
Wamorocco hao waliendeleza ndoto zao za kuchukua ubingwa wakiwa wenyeji baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Wabrazil jana, huku Ronaldinho akifunga bao zuri kwa njia ya adhabu na kufufua matumaini ya kutwaa ubingwa kama alivyofanya mwaka 2006 akiwa na Barcelona.



Mouchine Iajour aliifungia timu yake ya Raja bao la kuongoza kabla ya Ronaldinho kusawazisha, lakini Mouhcine Moutouali aliandika bao la pili dakika ya 84 kwa njia ya penati na Vivien Madibe aliwazamisha Wabrazil hao kwa kuandika bao la tatu .
Raja sasa itakumbana na mabingwa Ulaya, FC Bayern Munich siku ya jumamosi katika mchezo wa Fainali mjini Marakech




0 comments:
Post a Comment