Meneja
Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF) Bi. Eunice Chiume akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) mpango wa Shirika hilo kuendelea kutatua changamoto za makazi
kwa wanachama wake,wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara
ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi Zamaradi Kawawa.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
Na Georgina Misama
Shirika la Taifa la hifadhi ya jamii (NSSF) linaendelea na mikakati wa kutatua changamoto za makazi kwa wanachama wake.
Hayo
yamesemwa na Meneja Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa shirika hilo
Eunice Chiume wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam.
Eunice
alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa hitaji kubwa ya makazi shirika
limejipanga kukabiliana na changamoto hiyo kwa kuendelea kujenga nyumba
za bei nafuu zitakazouzwa kwa wanachama wake ili kuweza kuwapatia makazi
ya kudumu.
“baada
ya kukamilika kwa awamu ya kwanza naya pili ya ujenzi wa nyumba 297,
NSSF tumeona kuna haja ya kuendelea kukukabiliana na hali hii kwa
kuanzisha awamu ya tatu ya mradi wa nyumba za bei nafuu itakayohusisha
ujenzi wa nyumba 900 zitakazogharimu takriban shilingi bilioni 23.”
alisema Eunice.
Aidha
Eunice aliongeza kuwa kuanzia November 11 mwaka huu Shirika linatarajia
kuanza kutoa fomu za maombi ya kununua viwanja 498 vilivyopimwa katika
eneo la kiluvya A madukani, viwanja hivyo vitauzwa kwa ushirikiano wa
shirika na Halmashauri ya wilaya ya kisarawe, ambapo eneo hilo litakuwa
makazi mapya nay a kisasa litakalokuwa na huduma muhimu za kijamii.
Viwanja
hivyo vitauzwa kwa wanachama wa NSSF na jamii kwa ujumla kwa bei
inayoanzia Shilingi 15,000 hadi Shilingi 20,000 kwa mita ya mraba
kulingana na matumizi.
0 comments:
Post a Comment