
Na Mwandishi Wetu
BAADA
ya msanii Upendo Nkone kuthibitisha kushiriki Tamasha la Krismas
litakalofanyika Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,
msanii Upendo Kilahiro naye amejitosa kushiriki.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa
tayari wamefikia makubaliano na msanii huyo na wanafurahi kwamba tamasha
litaenda vile wanavyotaka.
“Kilahiro tutakuwa naye, naamini mwaka huu tamasha hili litakuwa bora zaidi kutokana na kushirikisha waimbaji wengi wakali.
“Mpaka sasa Watanzania wawili tumeshakubaliana nao, yaani Kilahiro na Upendo Nkone,” alisema Msama na kuongeza kuwa bado wanaendelea na mazungumzo na wasanii wengine wa nje na ndani ya nchi.
Baadhi
ya nyimbo za msanii huyo ni Zindonga alioimba kwa Kizulu), Unajibu
Maombi na Ni Salama Rohoni. Pia anatamba na albamu mbalimbali ikiwemo
Ficho Langu.
Tamasha
la Krismas linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es
Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Pasaka kila mwaka.
Waandaaji
hao wamepanga tamasha hilo lifanyike Desemba 25 Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam na siku inayofuata Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

0 comments:
Post a Comment