Na Mwandishi Wetu
WAANDAAJI
wa Tamasha la Krismas wametangaza kuwa asilimia 80 ya mapato
yatakayokusanywa kwenye tamasha hilo mwaka huu yatatumuka kwenye ujenzi
wa kito cha wasiojiweza Pugu, Dar es Salaam.
Tamasha
la Krismas linaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar
es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Pasaka kila mwaka linatarajiwa
kufanyika Desemba 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa asilimia nyingine
20 itatumika kulipia ada yatima wanaosoma shule mbalimbali hapa nchini.
“Asilimia
80 ya mapato tutaipeleka kwenye ujenzi wa kituo chetu cha wasiojiweza
tunachotarajia kukijenga Pugu, Dar es Salaam, huwa hatubahatishi
tunapodhamiria jambo letu,” alisema Msama.
Kwa
mujibu wa Msama, hivi sasa wanasubiri hati kutoka Wizara ya Ardhi
kuhusiana na umiliki wa eneo hilo na kwamba suala hilo litakapokamilika
ndipo mchakato wa ujenzi utakapoanza na wana imani jambo hilo
halitachukua muda mrefu.
Alieleza kuwa wakati wananzisha tamasha hilo mwaka 2000 dhamira yao ilikuwa kila mwaka kusaidia wasiojiweza.
“Niwashukuru
wadau mbalimbali waliotusaidia kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho na
mpaka sasa tuna karibu Sh milioni 120, ambapo gharama nzima ya ujenzi ni
kati ya Sh milioni 800 hadi Sh bilioni moja utakapokamilika.
“Dhamira
yetu ni kuwa na kituo ambacho kitasaidia Watanzania wa mikoa mbalimbali
ambao hawana uwezo katika masuala ya mavazi, elimu, vyakula na mengine
mengi,” alisema Msama.
Alieleza
kuwa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismas imeamua lifanyike
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Desemba 25 na siku inayofuata watatazama
mkoa gani waupe heshima.
Alisema
hilo litakuwa tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu na litakuwa na
tofauti kubwa iilinganisha na matamasha mengine yaliyowahi kuandaliwa na
kampuni yake.
0 comments:
Post a Comment