Baadhi
ya washiriki wa warsha ya viongozi wa kimila wa jamii ya ufugaji kuhusu
afya ya uzazi na kuzuia maambukizi ya ukimwi wanaonekana wakisikiliza
kwa makini mambo yaliyokuwa yakiongelewa kwenye warsha hiyo.

Baadhi
ya wafugaji wa jamii ya wamasai wakicheza ngoma za asili wakati wa
ufunguzi wa warsha hiyo kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar
tarehe 9.11.2013.

Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akifungua rasmi warsha ya siku moja ya viongozi wa kimila
wa jamii ya wafugaji kuhusu afya ya uzazi na kuzuia maambukizi ya ukimwi
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere hapa Dar tarehe
9.11.2013.

Mke
wa RaiS Mama Salma Kikwete akivishwa mavazi ya wafugaji wa jamii ya
wamasai wakati wa warsha ya viongozi wa kimila iliyofanyika Dar tarehe
9.11.2013. Baadaye Mama Salma alipokea zawadi kwa ajili ya Mheshimiwa
Rais Dkt. Jakaya Kikwete.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Oloiboni Bwana Tikwa Moreto wakati wa warsha.
0 comments:
Post a Comment