Mratibu wa Dawati la Magonjwa ya Milipuko na Maafa kutoka
Shirika la Afya Duniani (WHO) Dk. Grace Saguti akiwasilisha mada kuhusu
Sheria na Kanuni za Kimataifa za Afya kwenye semina ya wanahabari
jijini Dar es Salaam.

Mtaalamu
wa Masuala ya Epidemiolojia Dk. Vida Mmbaga kutoka Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii akiwasilisha mada kwenye semina hiyo.
Hussein Makame, MAELEZO
SHIRIKA
la Afya Duniani (WHO) limeitaka sekta binafsi kushikiana na Serikali
kutoa taarifa za magonjwa ya milipuko ili kukabiliana na athari za
magonjwa hayo ndani na nje ya nchi.
Hayo
yamesemwa na Mratibu wa Dawati la Magonjwa ya Milipuko na Maafa kutoka
WHO, Dk. Grace Saguti wakati akiwasilisha mada juu ya Sheria za
Kimataifa za Afya kwenye semina ya wanahabari iliyofanyika jijini Dar es
Salaam jana.
Alisema
kuwa kwa sasa dunia inakabiliwa na changamoto ya magonjwa mbalimbali ya
milipuko inayoenezwa kutoka ndani ya nchi na nje na kuathiri jamii ya
Watanzania lakini hayaripotiwi mapema ili kuyadhibiti.
Dk.
Saguti pia amewataka wananchi kutoa taarifa za magonjwa ya milipuko
pindi tu wanapoona dalili za magonjwa hayo ili kuyadhibiti na kuepusha
madhara yanayoweza kuenea katika sehemu kubwa ya jamii.
Kwa
upande wake Dk. Vida Mmbaga kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
alisema kuwa watu 10 walifariki dunia mkoani Rukwa kwa ugonjwa wa uti wa
mgongo kwa kipindi cha mwezi Oktoba mwaka huu.
Alisema
katika kipindi hicho wengine 34 waliugua ugonjwa huo ingawa hadi sasa
ni mgonjwa mmoja tu ndiye anayeugua ugonjwa huo huku baada ya Serikali
kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuelimisha
jamii kuhusu umuhimu wa kuwahi hospitali.
“Hatua
nyingi iliyochukuliwa ji kuelimisha jamii juu ya namna ya kudhibiti na
kuzuia ugonjwa huo, pia tulizuia mikusanyiko ya watu kwenye jamii, kutoa
matibabu na kushirikisha sekta mbalimbali katika kudhibiti ugonjwa huo”
alisema Dk. Mmbaga.
Aliwashauri
wananchi kuepuka misongomano yenywe watu wengi na iwapo mtu
atagundulika na dalili za ugonjwa huo akuwahi mapema kwenye vituo
vinavyotoa huduma ya afya ili kupata dhibiti ugonjwa husika.
Alisema
dalili kubwa za ugonjwa huo ni kukakamaa kwa shingo, homa kali, kuumwa
kichwa, na kutapika na kwamba asilimia 5 hadi 10 ya wagonjwa wanaougua
uti wa mgongo hufariki ndani ya saa ya siku moja au mbili.
Dk.
Mmbaga aliwataka watu wanaobaini kupata dalili hizo kwenye hospitali au
vituo vya afya na kuwatahadharisha ndugu wa mgonjwa kutomtenga mgonjwa
kutokana na kuugua ugonjwa huo.
0 comments:
Post a Comment